Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Tuesday, April 10, 2012

ALI KIBA KUTUZWA NA PRODUCER




ALI KIBA

PRODUCER MAN WATER KUMTUZA ALI KIBA.
Producer Man Water wa studio ya Combination Sounds nchini Tanzania, ameendelea na mpango wake wa kuwatuza wasanii mbalimbali waliorekodi ndani ya studio yake na nyimbo zao kufanya vizuri katka ulimwengu wa Bongo Fleva.


Kwa mujibu wa Man Water, mwaka huu atawatuza wa wasanii wawili Ally Kiba pamoja na msanii mwengine anayejulikana kwa jina Mbatizaji.


Man Water asema lengo la kufanya hivyo ni kutoa shukrani kwa wasanii, ambao kwa namna moja ama nyingine wameitangaza vyema studio yake na kumfanya yeye mwenyewe kuweza kujulikana na kupata kazi nyingi zaidi.


Alisema awali aliianza kwa msanii 20% na kumpa zawadi ya baadhi ya vyombo vya muziki na hivyo kwa mwaka huu yupo mbioni kumtunuku Ally Kiba ambaye wimbo wake kwa jina 'Dushelele' aliourekodi katika studio yake ya Combination Sounds imeweza kukubalika vilivyo na mashabiki wa muziki ndani na nje ya Tanzania.


“Kiba ni msanii mzuri na ni kati ya wanaoweza kuufanya muziki huu kuwa bora zaidi na kututangaza nje ya mipaka yetu kwa urahisi zaidi…..naamini nitaendelea kufanya kazi naye ili kuweza kutengeneza nyimbo zenye ubora zaidi na kuwaelimisha na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya,” alisema.
Akimzungumzia Mbatizaji, Water alisema atamtunuku msanii huyo kutokana na wimbo wake wa ‘Heshima ya Kazi’ kuweza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga, akisema ni mmoja kati ya wasanii wenye tungo zenye maadili na kufundisha jamii.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment