MR. TWO NA MKURUGENZI
WA CLOUDS FM WAPATANISHWA.
Hatimaye ugomvi wa Mkurugenzi wa Clouds Media (cloudsfmTz) Ruge
Mutahaba na Mbunge wa jimbo la Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA Joseph Mbilinyi (Mr. Two Sugu) umemalizika
baada ya kufanyika kwa vikao mbali mbali chini ya Waziri wa Habari Utamaduni na
Michezo wa Tanzania.
Hatua hii yatia kikomo ugomvi wa maneno makali na bifu
katika muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania uliopelekea kutochezwa kwa nyimbo
za kundi la Vinega na kutolewa kwa album mbili za kuwapaka matope wafanyikazi
mbali mbali wa Clouds Radio na Tv.
Baadhi ya wasanii wa Mombasani walikuwa wamejaribu kuiga bifu hii. Swali ni je kwa sasa watachukua hatua gani?
Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.
No comments:
Post a Comment