NANI ANAYEFAA
KUPEWA SHUKRANI BAADA YA MSANII KU’HIT KATIKA INDUSTRY?
Msanii hupitia
safari ndefu, akipitia mikononi mwa washikadau mbali mbali katika sekta ya
sanaa kabla ya ku’hit. Hata hivyo
baada ya msanii kuafikia ndoto yake ya kupata umaarufu na mafanikio ya kifedha
katika ulimwengu wa mziki, nani anafaa kupewa shukrani kufuatia mchango wake
mkubwa ama umuhimu mkubwa katika kufanikisha haya yote?
Wengi tuna majibu
tofauti kufuatia mitazamo yetu tofauti lakini ningeomba mwanzo huyu msanii
mwenyewe tumtoe katika orodha ya majibu yetu kwa sababu ni yeye tunamzungumzia
kwa leo.
Pili mwenyezi
mungu ambaye sote tunakubaliana kwamba ni mwezesha wa yote katika sanaa, mwanzo
wa kila kitu na ambaye hatupingi uwezo wake.
Sekta ya
sanaa hususan hapa Mombasani imetajwa kushirikisha washikadau mbalimbali
ikiwemo ma’producer,ma’promoter,ma’presenter na wasikilizaji. Washikadau
hawa hutekeleza majukumu mbali mbali na kuchangia kwa usawa katika kukua kwa
sanaa ya mziki. Hata hivyo wengi ya wasanii niliokumbana nao katika harakati za
kusukumu gurudumu la sanaa wameniuliza swali hili, “je tutakapo hit nani tumshukuru
zaidi?” Katika uchanganuzi wa washikadau katika jamii kupitia mchango wa
waskilizaji tukufu wa kipindi cha “Chipkizi Za Kaya”, tunapata picha kamili ya
majukumu mbali mbali ya washkadau wakuu katika sekta ya mziki wa Mombasani.
Producer hua mwanzo wa safari nzima ya msanii
na huchangia pakubwa katika kuasisi mafanikio ya msanii yeyote. Wengi ya ma’producer wetu huwa wajuzi wa sanaa ya
mziki mbali nakufahamu vyema jinsi ya kuruka viunzi tofauti tofauti katika mbio
za kutafuta mafanikio ya kimziki. Katika kipindi cha “Chipkizi Za Kaya” ndani
ya Radio Kaya jumapili ya tarehe 19, baadhi ya wasikilizaji waliotoa
michango yao kuhusiana na mjadala huu walimtaja producer kama kiungo muhimu
zaidi. Wengi walidai yeye ndio hupika chakula ambacho wao hutokea kukipenda.
Wakimlenganisha na mpishi jikoni, wengi wahoji kuwa producer nyakati zozote hushikilia funguo ya ufanisi kwa msanii
kwani yeye ndio ataamua kuongeza ama kupunguza chumvi katika chakula ambacho
msikilizaji ataamua kama nikitamu ama hakifai.
Promoter pia atajwa katika orodha ya
washikadau wakuu katika sekta ya mziki ambao pia huchangia pakubwa katika
ufanisi wa msanii hususan limbukeni ama anayechipuka. Promoter anasemekana kuwa
mfadhili wa ndoto nzima ya msanii. Kulingana mashabiki waliotoa mchango wao, promoter pia anaeza kulinganishwa na
mjasiriamali kwani katika mchakato mzima wa kumfadhili msanii, hua analenga
kufaidika baada ya msanii kufanikiwa kupitia pesa zitakazo kusanywa wakati wa ma’show. Kufuatia kutotaka kupoteza
mtaji alioekeza katika msanii, promoter
hufanya kila awezalo kuhakikisha msanii ana’hit
katika industry. Pia wengi washikilia kuwa promoter hua katika stage muhimu ya usanii. Stage ya uasisi wa ndoto nzima. Bila
yeye msanii huvunjika moyo na wengine
huachana na maswala ya mziki huku uwepo wa support
yake humtia moyo msanii kufanya bidii. Katika pointi hii msikilizaji mmoja
amfananisha promoter na mzazi kwa
mwanafunzi, ambapo humlipia fees na
kumuachia mwanafunzi jukumu la kutia bidii kufanikiwa.
Presenter tunazungumzia mtangazaji wa redio
ambaye hucheza wimbo wa msanii na kumtambulisha kwa mshikadau mwengine ambaye
ni msikilizaji. Wengi walisistiza ulazima katika kuwepo kwa uhusiano mwema kati
ya mshikadau huyu na yule awali kwa jina promoter.
Wasikilizaji wengi wadai uhusiano huu hua na mchango mkubwa katika jinsi msanii
atakavyowasilishwa kwa maskio ya waskilizaji. Kazi ya presenter kitaaluma huhusisha kuskiliza kazi za msanii na kuamua
iwapo zitawaburudisha wasikilizaji wake anapokua hewani. Jukumu hili alitwekwa
baada ya kubainika kwamba kufuatia uzoefu wake katika kazi, anaweza kujua ni
aina gani ya mziki msikilizaji wake hupenda. Baadhi ya waskilizaji waliochangia
mjadala huu pia walihoji kuwa presenter
hua na mamlaka ya kuamua kucheza ama kutocheza nyimbo. Jambo hili latajwa kumgeuza
na kuwa wa muhimu zaidi katika mafanikio ya msanii. Swala la mshikadau huyu
kuwa na uwezo wa kucheza ama kutocheza nyimbo hata anapoombwa na msikilizaji hewani
latajwa kumpa uzito zaidi katika ratili ya mchakato huu.
Msikilizaji ni yule anayeshabikia msanii katika redio.
Mara nyingi hushirikiana kwa sana na presenter
katika vipindi kabla ya kujiunga na mapromoter na msanii mwenyewe katika sehemu
za burudani. Mara nyingi hupiga simu kuomba wimbo ama kuketi chini na kuskiza
mziki unaochezwa katika kipindi. Kulingana na wengi waliochangia katika “Chipkizi Za Kaya” mshikadau huyu ni
miongoni mwa wale wakuu katika game,
kwani yeye ndiye anayetengenezewa nyimbo. Msanii anapo amua usanii lengo lake kubwa
huwa ni kumrai na kumfurahisha msikilizaji. Promoter anapoamua kumfadhili msanii hulenga kufaidika baadaye
msikilizaji huyu anapojitokeza katika sehemu za burudani kumwona msanii
mwenyewe.
Presenter humtegemea sana mshikadau huyu kimaisha
kwani yote anayofanya katika kazi yake hua ni kuhakikisha msikilizaji anafurahi
na kuganda katika kipindi chake kila uchao. Kwa vile msikilizaji anaamua mwenyewe
nyimbo gani inayo mfurahisha, presenter
mara nyingi hana budi bali kucheza wimbo ule msikilizaji anaoufagilia zaidi. Katika
muktadha huu, wengi ya walioshiriki mjadala huu walikubaliana kwamba shabiki huamua
ni nyimbo gani inayo hit. Mskilizaji
pia atajwa kuwafanya ma’promoter, ma’
presenter na ma’ producer kuwa busy kwani wote huwa katika harakati za kujaribu kumridhisha
mshikadau huyu. Umuhimu wake watajwa kuongezeka zaidi pale anapopewa nafasi na presenter kuchagua wimbo utakaochezwa
katika vipindi vya redioni.
Je nani
anayefaa kupewa shukrani baada ya msanii ku’hit katika industry?
No comments:
Post a Comment