Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Wednesday, March 21, 2012

BIFU KATI YA SUGU NA CLOUDS FM LARUDI TENA


MR TWO

SEASON 2 YA BIFU KATI YA ANTIVIRUS(VINEGA) NA CLOUDS FM YAANZA

Uhasama kati ya mbunge wa mbeya Mjini nchini Tanzania Joseph mbilinyi aka Mr. Two ( SUGU) na kituo kimoja cha redio nchini TZ (Clouds Fm) unaoonekana kujichipuza tena.

Haya yanajiri wiki chache baada ya sugu na kundi lake la wasanii waliotoa album mbili za kupaka matope kituo hichi na watangazaji wake (Anti Virus vol 1 & 2 ) kupatanishwa na usimamizi wa kituo hicho chini ya waziri mmoja wa serikali ya Tanzania.

Sugu na kundi lake walianzisha vita na kituo cha Clouds Fm – Radio ya watu kufuatia madai ya nyimbo zao kutochezwa katika kituo hichi ambacho kinaongoza nchini Tanzania kwa waskilizaji na pia madai ya rushwa dhidi ya watangazaji wa kituo hicho.

Sugu na kundi lake wametuma ujumbe huu kwa vyombo vya habari, wakielezea sababu ya kuanza tena kwa uahasama baina yao;


HAKIKA TUMEPITIA MENGI MACHUNGU NA HATUJAKATA TAMAA.JAMANI TUELEWE JAMBO MOJA TU, NAFASI YA AMANI NDIO INAYOTAFUTWA POPOTE DUNIANI NA KIZURI NI KWAMBA ADUI NDIO ANANYOOSHA MIKONO JUU KWA KUTAMBUA HARAKATI ZA MUZIKI KWA VIJANA WA TAIFA HILI. TUMEKOMALIA MAMBO AMBAYO TUNAAMINI NDIO MIZIZI YA UFISADI NA UKANDAMIZAJI WOTE UNAOFANYWA NA WAFU FM PAMOJA NA WANAOSHIRIKIANA NAO (majina kwenye vol 3).

WAMECHOMOA NA KUYAKATAA MAKUBALIANO YOTE BAADA YA KUKUBALI HAPO AWALI MBELE YA WAZIRI, KUPITIA KIKAO CHA UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO HAYO MBELE YA VIONGOZI WA BASATA WALIOKUWEPO(ushahidi wa sauti za kikao upo na tutautoa).

WAMEAMUA KUTURUDISHA VITANI NA HAYA NDIO MAISHA YETU.....NA KILA MMOJA WETU ANASHANGAA JAMAA SIJUI NI NANI ANAYEWASHAURI KWANI WALILETA SHAURI LA KUITWA MAHAKAMANI KWA WATU 7 AKIWEMO;

1. SUGU (aliyekamatwa mara kadhaa na kupelekwa makao makuu ya usalama wa taifa,jukwaa la wahariri,police n.k)
2. DANI (anayetafutwa na aliyetishwa mara kadhaa n.k)
3. MKOLONI (aliyewahi kuwekewa sumu ili kuuwawa,aliyeenda usalama,police,kwa Mh Waziri,anayetafutwa n.k)
4. RAMA D (anayetafutwa na ambaye nyumba yake iliingiliwa na polisi usiku usiku n.k)
5. ADILI(ambaye alikamatwa na kupelekwa police central kwa harakati hizi na watu bado tulisimama tukalimaliza)

NA SIO MAPACHA (wanaotafutwa n.k) PEKEE KAMA WATU WANAVYODHANI NA TAARIFA HIZO SIJUI NI KARANI YUPI(mpumbavu) KAZIPELEKA BAR INAITWA MLIMANI JIRANI NA ILIPO KAMBI YETU KAMPATIA MHUDUMU ANAITWA MAEDA.

ULIWAHI KUSIKIA WAPI KITU KAMA HIKI?? ETI SUMMARCY ZA MAHAKAMA ZINAPELEKWA KWA COUNTER WA BAR?

KWA HIYO TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA WAELEWE KUWA CLOUDS FM WAMETURUDISHA VITANI RASMI NA KWA UFUPI TUPO KAMBINI WATAHUSUDU..................VOL 3 COMING OUT SOON!!!!!!


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment