JIMMIE GAIT AKANA KUWA SHOGA
Msanii wa mziki wa injili nchini Jimmie Gait ameamua kuzima
uvumi ambao kwa mda umesheheni katika mitandao ya kijamii, kuhusiana na "sexuality"
yake, ambapo wengi wameelezea wasiwasi wao kwamba huenda akawa ni shoga.
Karibuni kumejitokeza mwanamume mmoja shoga ambaye amedai
kwamba amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii huyu wa nyimbo za
injili.
Hata hivyo jimmie gait amejitokeza na kuweka wazi kwamba ana
mchumba wa kike ambaye wame date kwa mda mrefu anayempenda sana na kuelezea
kutoshangazwa kwake na uvumi huo kwani si mara ya kwanza maishani mwake amekuwa
akifuatwa na mashoga waliotaka awe na uhusiano nao.
Gait pia aweka wazi kwamba hawachukulii vibaya wanaume
mashoga na pia akaitaka jamii kuheshimu maisha yake yakibinafsi.
Kwa mengi Zaidi usikose
kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani
Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd
- "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.
No comments:
Post a Comment