BAADA ya kumtoa Bi Cheka, msanii wa muziki wa kizazi kipya
kutoka TMK, Mh Temba, amesema kuwa anatarajia kutoa ngoma yake mpya inayokwenda
kwa jina la ‘Mazoea’, ambayo itatoka sambamba na video yake.
Msanii huyo ambaye
amekuwa mstari wa mbele kuwatoa nyota chipukizi, asema wimbo huo ndiyo
utakaokuwa wa kwanza kwa upande wake na anaamini utakuwa moto wa kuotea mbali.
Alisema kuwa ngoma
hiyo haitakuwa kuwa na mfano kwani muziki wake anafanya tofauti na wasanii
wengine hivyo mashabiki wake wake mkao wa kula kuweza kuupokea ujio wake mpya.
“Hiyo ndo ngoma yangu mpya ambayo ambayo itakuwa sokoni
April mwaka huu hivyo nawaomba mashabiki wangu wawe na uvumilivu kwani sitaki
kufanya kitu kwa haraka baada nije kuharibu,” alisema..
No comments:
Post a Comment