Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Wednesday, March 21, 2012

BOB JUNIOR KUACHILIA VIDEO YA WIMBO MPYA KABLA YA AUDIO





BOB JUNIOR KUACHILIA VIDEO HALAFU BAADAYE AUDIO YA WIMBO WAKE MPYA "NIMCHUMU"

Msanii mkali wa mziki wa Bongo fleva ambaye pia ni producer Bob Junior, afichua kuwa anapanga kuachilia video ya wimbo wake mpya kwa jina “Nichumu” kwanza kabla ya kusambaza "audio" kwa vituo vya redio



Akizungumzia wimbo huo, msanii/producer huyo adai kuwa katika ngoma hiyo ameimba zaidi kuliko nyimbo zote alizowahi kuzitoa na anaamini mashabiki wa bongo fleva watakapouskia hawatachoka kuuskiza tena na tena.



Bob Juniour asema kikubwa alichokiimba ndani ya kazi hiyo ni mapenzi ambayo anaamini hayana kikomo na mwisho wa kupenda ni pale mungu atakapokuchukua.



“Hakuna asiyejua raha ya kupendwa hivyo hii ni ngoma ambayo imejaa mapenzi na naamini  mashabiki wangu wataipenda kutokana na ubora wake,” alisema.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

1 comment: