Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Tuesday, April 24, 2012

BI. CHEKA AITWA MCHAWI

                  
BI. CHEKA AWAHI KUITWA MCHAWI.
Ajuza ambaye kwa sasa anapeta sana katika mziki wa kizazi kipya nchini Tanzania baada ya kufanya wimbo na Mh. Temba wa kundi la TMK, Bi. Cheka afichua kuwa kabla ya umaarufu wake wa kimziki aliwahi kuitwa mchawi.

Bi. Cheka asema kabla ya kuanza usaniii aliwahi kufanya biashara ndogo ndogo ikiwemo kuuza mahari mataani ambapo baadhi ya majirani wake walimvumisha kuwa mshirikina aka mchawi kufuatia uzee wake.

Bi. Cheka hata hivyo hajachelea kuwasamehe majirani wake ambao kwa sasa wameanza kubadilisha mitazamo yao kumhusu baada ya kupata mafanikio katika ulimwengu wa Bongo fleva.
        

Hata hivyo Bi. Cheka pia awanyoshea kidole cha lawama adui zake mtaani ambao bado hawajafurahishwa na hatua yake ya kimafanikio katika ulimwengu wa kimziki, kufuatia kile alichokitaja kama ugonjwa usiojulikana sababu yake ambao uliokumba wiki iliyopita.

Bi. Cheka adai ilibidi kupata matibabu kutoka kwa babu mmoja aliyempa miti shamba kuweza kumponya ugonjwa huo ambao hadi sasa haujabainika chanzo chake.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment