DUDUBAYA KUHAMA DAR ES SALAAM KARIBUNI.
MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini aka Dudubaya anaeishi area 88.4
Dar es salaam nchini Tanzania, ametangaza rasmi kupitia mtandao mmoja wa
kijamii kwamba anajipanga kuihama Dar es Salaam na kwenda kuishi kwao Kiseza huko
Mwanza katika kipindi cha miaka mitatu
ijayo.
Dudubaya asema sababu mbili kubwa zinazomfanya kuuhama mji
mkuu wa Tanzania Dar es Salaam na kuelekea mkoa wa Mwanza ni joto na jam za barabarani, ambazo amedai
humchelewesha kila mara .
Dudubaya ambae alianza maisha ya kujitegemea jijini Dar es
salaam miaka saba iliyopita, amesema kwa sasa anakaribia kumalizia nyumba yake
anayoijenga nyumbani kwao Mwanza, ambayo
anadai imemgharimu shilingi milioni kumi pesa za Tanzania.
Kwa sasa Dudubaya anamiliki kampuni moja inayojihusisha na kuuza madirisha
na milango ya mbao, pamoja na kampuni ya kuandaa show za wasanii kwenye mikoa
mbalimbali ya Tanzania hukuakijihusisha na ulimwengu wa filamu za kibongo pia.
Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.
No comments:
Post a Comment