Mr. Bado a.k.a
Mzungugiryama
Ni Msanii aliyezaliwa huko Malindi
sehemu ya Watamu katika kaunti ya Kilifi. Alizaliwa mnamo tarehe 15 Desemba
mwaka wa 1980. Ni mwana wa msanii Maarufu wa ngoma za kitamaduni za jamii ya Wamijikenda;
Mzee Nyerere Wa Konde na Mama Mariam Mohammmed. Ni mtoto wa tano katika
familia hii iliyojaliwa watato 10.
Mr. Bado a.k.a
Mzungugiryama ambaye majina yake halisi ni Mohammed Said Ngana, alipata masomo yake ya msingi
katika shule ya msingi ya Gede Primary School kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Barani Secondary School
mjini Malindi.
Mr. Bado afichua kuwa usanii wake ulianza
kitambo na babake Mzee Nyerere Wa Konde alichangia
pakubwa katika yeye kupenda maswala ya mziki na utumbuizaji. Mr. Bado anakumbuka kwa madaha kisa ambacho kilichootesha ari yake ya
kuwa mwanamziki. Mr. Bado anasema aliwahi kutumbuiza umati
mkubwa akiwa na umri mdogo, ambapo ilikuwa ni mwaka wa 1990 wakati wa matanga
ya marehemu nyanyake. Babake ambaye alikua anatumbuiza umati kwa nyimbo zake za
kimijikenda alimshika mkono na kumvuta mbele ya umati akimtaka amsaidie katika
kutumbuiza watu.
Hata hivyo alianza maswala ya mziki hususan wa kizazi kipya
“seriously” mwaka wa 1996 na toka mwaka huo hadi sasa anasema ari yake ya
kutaka kufanikiwa kimziki haijawahi kufifia.
Wimbo wake wakwanza uliomtambulisha kwa mashabiki wa “ngomapwani”
anasema ni “Stand By Me
“ aliourekodi mwaka wa 2005 katika studio za FP Records chini ya
uangalizi wa “Producer” Fleva, huku
akifichua kua show yake ya kwanza ya kutumbuiza mashabiki iliandaliwa katika
mkahawa wa Happy Nights mjini Watamu.
Kwa sasa amekuja na kibao kipya kiitwacho “Machozi”
akimshirikisha mwanadada kwa jina Shamim
a.k.a Shamo, kilichoimbwa kwa lugha ya Kiswahili na kiarabu na kurekodiwa
katika studio ya Bado Records, inayopatikana mjini Watamu katika kaunti ya Kilifi mkoani Pwani.
Mr. Bado afichua kuwa mwadada huyu kwa jina
Shamim a.k.a Shamo ni dadake mdogo
na ushirikiano huu ulikuwa wa kum’introduce kwa “game” ya Mombasani. Mr. Bado afichua kuwa familia yao
imejaa wanamziki na mwadada huyu ni nduguye wa pili kujiunga na mziki baada ya
kakake mkubwa Nyerere Juniour, ambaye ni msanii wa nyimbo za
kitamaduni na babake Nyerer e Wa Konde.
Mr. Bado afichua kuwa karibuni anatarajia kusafiri
ng’ambo na angependa kumwacha dadake mdogo akiendeleza ndoto ya mziki, ambayo amefichua
kuwa ni sawa na urithi wa kifamilia.
Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.
MR. BADO & SHAMO - MACHOZI
Contacts:
http://www.facebook/Bado
Mzungugiryama
badotalents@gmail.com
No comments:
Post a Comment