WASANII WA MADAWA YA KULEVYA WATAJWA.
Kifo cha malkia wa muziki wa Pop, RnB na Soul wa Marekani,
Whitney Elizabeth Houston kilichochangiwa na matumizi ya madawa ya kulevya, chaibua
mchakato mpya ambapo imepelekea kutolewa kwa orodha ya wasanii wa bongo flavaz wanaodaiwa
kwa watumizi wa Mihadarati. Mihadarati iliyotajwa ikiwa ‘unga’, bangi, miraa na
aina nyengine.
Habari za chini kwa chini zinadai kuwa kwa sasa mastaa kibao wanatumia madawa ya kulevya huku majina makubwa kama Msafiri Sayai ‘Diouf’, Albert Mangwair, Langa Kileo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Aisha Mbegu ‘Madinda’, Khaleed Mohamed ‘TID’, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’, Abas Kinzasa ‘20%’, David Nyika ‘Daz Baba’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Happiness Thadei ‘Sister P’ na Rose Ndauka yakitajwa.
Katika orodha hii Fid Q ndiye msanii wa pekee aliyejitokeza
wazi wazi kukana madai haya.
Huku sanaa ya bongo flavaz ikiimarisha juhudi za kukabiliana
na tabia ya utumizi wa Mihadarati miongoni mwa wasanii wa Bongo, wakereketwa wa
mziki wa Mombasani pia wahimizwa kuiga juhudi hizi ili kumaliza tabia hii
miongoni mwa wasanii wa mkoa wa pwani.
Niwazi kwamba kuna baadhi ya wasanii wa pwani ambao
wameonekana wazi wazi wakitumia madawa mbali mbali katika sehemu za burudani
hususan kabla ya kufanya performance.
No comments:
Post a Comment