KLEANHEART
Emmanuel Ogutu a.k.a Kleanheart ni msanii wa Hip Hop
na R&B kutoka mji wa Malindi
{Chocolate City} ambaye alianza safari yake ya mziki mwaka wa 1997 akiwa katika
kikosi cha “Akraba” wakiwemo na wasanii wengine “Jix” na “Mc Diddy.”
Amekuwa nyuma ya pazia ya muziki huku mashabiki wake
wakiwa na hamu yakutakakujuwa chanzo cha kimya chake. Akifichua sababu yenyewe
Kleanheart asme masomo yalikosa kumpa nafasi ya kushughulikia mziki hadi pale
alipo maliza kidato cha nne mwaka wa 2006.
Ni mzaliwa wa mji wa Malindi Kisumu-Ndogo na alisomea
shule ya msingi ya Malindi Primary school(HGM) kabla ya kupata elimu ya upili Kakuyuni
Secondary. Hajaoa yupo “single” na ni mtoto wa tisa katika family ya Mama Nora
Ogutu na Mzee Ogutu Atata babake ,ambaye ni marehemu kwa sasa.
Hali yake kama Mlemavu ni changamoto pia katika
maisha yake ya kisanii japo ndoto zake ni kubwa na zinamuacha na matumaini
mengi. Klean heart alidondosha vibao kama “Tabia za madem”, “Naitwa pesa,” “Nipe
nafasi” na pia kushirikishwa katika kolabo mbalimbali kama “Take it slow,”
aliyoifanya na msanii GRA, “Marina” ya msanii Musha, “Joy” ya msanii Escobar miongoni mwa nyenginezo.
Ni mmiliki mkuu wa Heartland Films kampuni inayo
shughulika na filamu na video za muziki mjini Malindi. Pia anahusika na
utayarishi wa gazeti la kila mwezi ambalo karibu litakuwa nje kwa jina MTAZAMO
MAGAZINE.
Kwa sasa Kleanheart ametoa wimbo mpya kwa jina "CHEMCHEM ZA KISANII " ajia kutoka kwa albam yake ya
pili kwa jina “AKILI KICHWANI".
Anawaomba mashabiki wamshike mkono katika safari
ndefu ya muziki huku akiwaahidi mambo mapya kila uchao.
Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz
a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" -
"Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu
Cha Umoja Wa Pwani ™.
No comments:
Post a Comment