Sir Malcom P |
R.I.P SIR
MALCOM P
Wakereketwa
wa mziki Mombasani leo waadhimisha miaka miwili tangu kuondoka kwa msanii
maarufu katika ukanda wa pwani Sir Malcom P.
Malcom P
ambaye majina yake halisi ni Malcom Puga, alifariki siku kama ya leo mwaka wa
2010 kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika barabara kuu ya Likoni - Lungalunga
Marehemu alikua
ametoka nyumbani kwake Ukunda akielekea Kaloleni katika mkahawa mpya wa Kings
ambako alikua anaenda kusherekea siku ya kuzaliwa kwake na alikuwa anafikisha miaka
35
Malcom P alikuwa
meneja wa wa klabu ya Kings – Ukunda na Kings Recording studio na alikuwa
amaefungua mkahawa mpya njini Kaloleni uliokuwa pia unaitwa Kings – Kaloleni.
Jumatano ya
tarehe 24.02.2010 daima itabaki katika kumbukumbu za wakereketwa wa game ya
Mombasani, kwani ni siku waliyompoteza kigogo wa game aliyekuwa ameshika
mikono na kuwaenua wasanii na maproducer mbalimbali pwani, mbali na kufanya kazi
zilizokubalika na wasanii wa taifa jirani la Tanzania.
Msanii
Malcom P aliwahi kufanya kazi na kundi la TMK family, PNC na Yakuza Mobb.
Kwa mengi
Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari
Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm
Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.
No comments:
Post a Comment