BELLE9
APINGA KUIBA WIMBO WA SLIM G - NAJMA
Baada ya kusalia kimya kwa mda msaanii mkali nchini Tanzania Abednego Damien aka Belle9 ameamua kujibu madai yalioshamiri
katika vyombo vya habari nchni Kenya,
kwamba kuna wimbo alimuibia msanii kutoka Kenya kwa jina Slim G, wimbo unaojulikana kwa jina Najma.
Akizungumza na Kaya
Flavaz jijini Dar Es Salaam, Belle9 asema kuwa wimbo ambao unazungumziwa siwake na
kufichua kuwa hajawahi kuimba wimbo kwa jina Najma. Belle9 asema kuna kipindi flani miaka ya nyuma aliwahi kusikia
story kama hizo lakini baada ya ufuatilizi akagundua wimbo huo uliimbwa na msanii
mwengine ambaye sauti yake imefanana sana na yake.
Belle9
asema tatizo hili limechangiwa na “pirates”
ambao waliubatiza wimbo huu jina lake na kupelekea wimbo huo kusambaa ukiwa na
jina la belle9 kupitia cybercafés zinazo
burn mziki.
“Nyimbo zangu nilizoziimba mashabiki wangu
wanazifahamu kutoka na utunzi wa
mashairi na style yangu kutoka enzi za Mapenzi ya sumu, Masogange We ni Wangu,
Nilipe ni Sepe hadi sasa Nimerudi , ambayo ndio single yangu mpya” akasema
Belle9.
“Kama hizi story ni kweli basi wangekuwa wamewahi
kuniskia nikiu’peform wimbo huo.Lakini waliokuja kwa shows zangu Mombasa wanaweza
kuwa mashahidi wangu. Sijawahi kuimba wimbo kama huo”.
Utafiti wa kayaflavaz wagundua kwamba original copy
ya wimbo huu unaozungumziwa ulisave’iwa Kwa jina “NEIGHBOUR _-_NAJMA fullvision”. Na zaidi ya yote wimbo huu hauna "intro" wala "outro" inayotaja jina la studio wimbo ulikorekodiwa ama jina la msanii aliyeuimba, kinyume na nyimbo nyingi za wasanii wa kizazi kipya.
Belle9 hata hivyo hakuficha kughadhabishwa kwake na
jinsi Slim G alivyoshughulikia utata huu
na kumlaumu kwa kuamua kwenda kwa media bila hata ya kuskia upande wa
Belle9.
Zaidi ya yote Belle9
ashkuru Kaya Flavaz kwa kufanya juhudi za mchwa kumtafuta ili kuskia upande wake
wa mtafaruku huu wote na kuelezea kushtushwa kwake na jinsi vituo kadhaa vya
redio jijini Mombasa vilivyoshughulikia story hii.
Belle9 awaomba msamaha mashabiki wake kwa mtafaruku
uliotokea na kufichua kwamba bado ataendelea kuwatumbuiza na nyimbo kali kali.
Hii si mara ya kwanza kwa “pirates” kulaumiwa katika kubadilisha majina ya nyimbo za wasanii. Itakumbukwa kwamba msanii Uncle
Chonia pia alijipata katika hali hii baada ya wimbo
wake maarufu “Merimela” kusambaa na
jina la msaniii Sudi Boy wa mombasani katika video.
Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz
a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" -
"Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu
Cha Umoja Wa Pwani ™.
No comments:
Post a Comment