Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Friday, March 16, 2012

DIAMOND KUIMBA TAARAB


DIAMOND
DIAMOND AFIKIRIA KUBADILI STYLE YA MZIKI HADI TAARAB


Naseeb Abdul aka Diamond msanii anayevuma kwa sasa nchini Bongo afichua kuwa anafikiria kubadili style ya nyimbo zake nakuingilia mtindo wa taarabu.


Diaomond asema haya yanamfika akilini mwake baada ya kukosa mpinzani kwenye style ya bongo fleva nchini Tanzania.


Diamond asema katika maisha yake ya kimziki hakuna msanii ambaye anaweza kufikia kiwango chake kisanii . Diamond ataja hatua ya nyimbo zake kuhit bila ya kumshirikisha msanii mwengine kama inshara mojawapo ya ukali wake katika ulimwengu wa Bongo flevaz.


Diamond asema kinachomfanya kufikiria kufanya kila aina ya muziki ni kipaji alichonacho, kwani  anaamini kuwa hashindwi na chochote kufuatia uwezo wake wa kisanii.


Msanii huyo aongeza kuwa bado hajaamua kufanya muziki huo rasmi lakini anafikiria kama unaweza kumletea soko kama ilivyo mziki wa bongo fleva, ambao umemfanya ajulikane duniani kote.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment