BIFU KATI YA ROMA MKATOLIKI NA IZZO BIZNESS LANUKIA
Msanii mkali wa hip hop kutoka Mbeya nchini Tanzania Izzo
Bizness aonekana kujiaanda kwa bifu dhidi ya rapper mwengine mkali katika
ulimwengu wa Hiphop nchini Tanzania Roma Mkatoliki, baada ya kumshambulia kwa
maneno akiwa jukwaani anaperform.
Izzo Bizness adai yeye yuko juu ya Roma Mkatoliki kimziki na
kamwe hakuna hata siku moja atamfikia kimashairi.
“Roma ni mdogo sana kwangu na mimi ni mkubwa kwake, hii
imekaa kihiphop kwa sababu kwenye hiphop kuna kupishana kauli kama hivyo”
Uhasama huu wakisanii waonekana kupigwa pondo na wasanii
wengine baada ya Suma Lee kuweka wazi msimamo wake kuhusiana na hali ya
kutofautiana kimziki kati ya wasanii hawa wawili.
Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.
No comments:
Post a Comment