Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Thursday, March 1, 2012

JE “BIFU” ZINASAIDIA WASANII?



JE “BIFU” ZINASAIDIA WASANII?

Historia ya muziki wa kizazi kipya haiwezi kukamilika pasipo kutaja matukio ya uhasama kati ya baadhi ya wasanii wa muziki huo.Pengine neno ‘uhasama’ halileti ladha ama kuzua hisia zaidi katika ulimwengu wa mziki wa kizazi kipya.Neno ‘bifu’, linalotokana na ‘beef’ ambalo ni slang ya Kiingereza cha Wamarekani  Weusi, ni neno ambalo wengi hulitumia kuashiria uhasama kati ya wanamziki hususan wa kizazi kipya hapa mombasani.

Mwandishi mmoja wa gazeti la Daily Mail la Uingereza aliwahi kuandika kuwa ‘vituko katika fani ya muziki wa hip-hop na rap ni miongoni mwa chembechembe muhimu kwa mafanikio ya msanii wa muziki huo’. Alitaja vituko hivyo kuwa ni pamoja na bifu. Iwapo bifu zinasaidia uhai wa hip-hop na rap au zinadidimiza, mie sina jibu bali kwa namna moja au nyingine zimewasaidia baadhi ya wasanii kufanya vizuri katika mauzo ya albamu zao.

Katika mjadala wa kubainisha iwapo bifu ama uhasama baina ya wasanii husadia ama kutosaidia kukua kwa sanaa ya mziki mombasani, washikadau wakuu wa mziki wa kizazi kipya (mashabiki) wachora mitazamo tofauti.


WALIOUNGA MKONO.

Katika Kipindi cha Chipkizi Za Kaya Jumapili iliyopita Walioegemea mtazamo kwamba bifu husaidia wa hoji kwamba tabia ya uhasama baina ya wasanii ni utamaduni wajadi hususan katika ulimwengu wa mziki wa Hiphop. Uhasama huu watajwa kuongeza umaarufu wa wasanii husika kwani waskilizaji hugawanyika na kuamua ni yupi kati ya wasanii wawili wanaolumbana watawashabikia. Hii huzua na kujenga mashabiki sugu wa wasanii husika, ambao wanaweza kufananishwa na mashabiki sugu wa timu za soka. Kuna imani miongoni mwa baadhi ya wapenzi wa hip-hop na rap kwamba bifu kati ya wasanii marehemu Tupac Shakur na Notorious B.I.G ilisaidia sana kuongeza umaarufu wa wasanii hao.

Bila shaka wafuatiliaji wa bongoflava wanakumbuka bifu kati ya Juma Nature na Inspekta Haroun na ile ya wasanii wa East Coast Team na wale wa maeneo ya Temeke. Japo haifahamiki vizuri historia ya bifu hizo mbili, lakini kwa hakika zilivuta hisia za wapenzi wengi wa bongoflava.Hapa mombasani mbali na kupanda kwa joto la kisiasa mwaka wa 2007 uhasama kati ya wasaani waliokua juu nyakati hizo Rudeboys na msanii aliyekua anachipuka Susumila yatajwa kuchangia kupanda kwa umaarufu wa Susumila miongoni mwawakereketwa wa fani ya Mombasani. Jijini Nairobi kupanda kwa umaarufu wa Octopizzo watajwa kuchangiwa sana na uhasama baina yake na msanii mkongwe wahiphop Abbas Kubaff, huku bifu kati ya Bamboo na wafuasi wa kundi la Klepto pia latajwa kuchangia kutambulika kwa baadhi ya wasanii wa kundi hilo.
Tabia hii pia yatajwa kuongeza mauzo ya album katika mataifa yaliyoendelea. Bifu kati ya msanii Rick Ross na 50 Cent nchini marekani inaaminika kuchangia mauzo mazuri ya albmu ya Rick Ross inayofahamika kama ‘Deeper Than Rap‘.

Hata hivyo,kama kweli bifu zinasaidia maendeleo ya wasanii, kwanini basi marapa kama Ja Rule na Fat Joe ‘wamepotea’ licha ya bifu lao na 50 Cent huku Benzino akibaki historia baada ya bifu lake na Eminem?Au ili bifu lizae matunda ‘yanayokusudiwa’ sharti wahusika ‘waimudu’(kama Rick Ross alivyoweza ‘kustahimili’ bifu lake na 50 Cent)?Lakini kama suala ni ‘kumudu bifu’ mbona Jadakiss ameweza ‘kusimama vizuri’ hata baada ya ‘kupatana’ na 50 Cent?

Wakichangia mjadala huu katika kipindi cha Chipkizi za Kaya, baadhi ya wasikilizaji pia wasema amani haiji ila kwa ncha ya upanga na kinachofuata baada ya uhasama huu  huwa mapatano na heshima. Uwepo wa heshma katika sanaa ya mziki kunachangia kukua kwa mziki kwani mipaka baina ya wasanii mbali mbali huwa wazi na kazi zao ndizo zinazowawakilisha kwa mashabiki wao.

WALIOPINGA;
Msemo wa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu ulikua kauili mbiu ya wengi waliopinga kwamba uhasama husaidia sanaa ya mziki wa kizazi kipya. Bifu yatajwa kuleta mgawanyiko si kwa wasanii wahusika pekee, bali hata kwa mashabiki. Hali hii yatajwa kusabaratisha baadhi ya wasanii na kupeana nafasi kwa wasanii wachache kupata mafanikio ya kimziki pekee kwa mda mrefu.

Kusambaratika kwa kundi la ECT na TMK baada ya bifu yao kwatajwa kama mfano. Bifu kati ya wasanii wa iliyokuwa East Coast Team na wale wa Temeke ilikufa kitambo kama ilivyotokea kwa bifu kati ya Nature na Inspekta. Lakini cha kushangaza, sio tu kwamba bifu hizo zilikwisha bali pia kulijitokeza mabadiliko makubwa kuhusu wasanii waliohusika na bifu hizo.

East Coast Team ilisambaratika huku wanakundi MwanaFA na AY wakitangaza kufanya kazi zao za kisanii kibinafsi (na wameendelea kuwa na mafanikio makubwa) lakini majina kama King Crazy GK (kiongozi wa kundi hilo) na O’Ten yamebaki kuwa historia tu.Kwa wenzao wa Temeke, japo kulizuka bifu jingine kati ya Wanaume Family na Wanaume Halisi baada ya kundi la Wanaume kugawanyika, kinachoweza kupigiwa mstari zaidi ni ‘kupotea’ kwa Nature na Inspekta katika anga za bongofleva.Ikumbukwe kuwa wasanii hao wawili walifikia hatua ya kupatana bbadaye na kushirikiana katika kundi la Wanaume Halisi.

Wanaoshuku mtazamo kwamba bifu hupelekea kupanda kwa mauzo ya album za wasanii wahusika wapiga mfano wa kudorora kwa mauzo ya album ya 50 Cent ya ‘Before I Self Destruct‘  licha ya uwepo wa bifu kubwa na msanii mwengine Rick Ross?

Udogo wa game ya Mombasani pia watajwa kutoweza kuwafanikisha wasanii wenye bifu. Uchache wa mashabiki wazua ugumu wa kuwaganya kwani hata wakigawanywa wale ambao msanii atawapata hawawezi kumfaidisha.Kutokuwa na utamaduni wa mashabiki kununua album madukani ama kupitia mtandao pia kwatajwa kutowafaidisha wenye bifu kwani uhasama wao hutajwa tu maredioni na hakutakua na faida kwao. Pia mashabiki wasema Ifikiapo hapa huhitajika utayari wa washikadau wa vyombo vya habari kuzungumzia bifu hili kuwafikia mashabiki lakini isipokuwa hivi, bifu hili huishia mitaani likijulikana na wasanii wenyewe tu na marafikizao wa karibu.

Wengine wasema ili ufanisi upatikane kutokana na bifu, kunahaja ya wasanii wote kuhusika vilivyo katika uhasama huo. Msanii mmoja anapompuuza mwengine na kuamua kutomjibu mwenzake katika malumbano hususan ya nyimbo na katika mahojiano, hupunguza makali ya mchakato mzima wa bifu na kupunguza utamu. Kutojibiwa kwa msanii Daddy Q na msanii susumila wakati bifu baina yao Mombasani kwatajwa kutompa nafasi Daddy Q kupata umaarufu, huku hatua ya rudeboyz kumjibu susumila kukionekena kama hatua iliyosaidia kupatikana kwa umarufu kwa uhasama baina yao na pia kusambaa kwa jina la msanii susumila.

Je kufikia hapa inatosha kusema kuwa bifu ni jambo jema au baya kwa sanaa ya muziki? Mie nimechokoza mjadala tu, nakuachia wewe msomaji uuendeleze nauamue.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.


©mwanamgambo2012

No comments:

Post a Comment