Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Thursday, May 3, 2012

CHIDI BENZ AZUNGUMZIA KUTOBOA PUA




“NIMETOBOA PUA KUONYESHA HISIA” - CHIDI.

Msanii wa Hiphop Bongo flava kwa Rashid Jumanne a.k.a CHID BENZ amezua hisia tofauti miongoni mwa wakereketwa wa mziki wa Bongo Flava hususan wanaume baada ya kuamua kutoba pua yake.

Hata hivyo akizungumzia hatua aliyochokua, kiongozi huyo wa kundi la 'LA FAMILIA' lenye maskani yake Ilala jijini Dar Es Salaam aeleza aliamua kutoboa pua (kutoga) ili kuonyesha hisia za maumivu aliyoyapata miaka iliyopita. 
CHID BENZ asema kwa muda amekua akiumizwa katika nyanja za mapenzi, safu nyenginezo na aliona bora atoboe pua ili apate maumivu, ambayo kwake itabakia kuwa kumbukumbu.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment