Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Monday, May 7, 2012

ROMA KUTOA "DOCUMENTARY" YA MAISHA YAKE.


ROMA 
Mwanahiphop bora kwa mwaka 2012, Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki ako katika harakati za kutengeneza documentary”  itakayoelezea maisha yake ya mziki tangu alipoanza hadi alipofikia sasa. 

Roma ambaye anatamba na kibao Mathematics asema kuwa documentary hiyo itaweka wazi maisha yake aliyoyapitia pamoja na vikwazo alivyovipitia. 

"DVD hii inatengenezewa hapa katika studio za Tongwe Records na ni mapema sana kusema kuwa itatoka lini ila haitochelewa kutoka na naamini watu wataipenda na italeta utofauti kidogo maana story iliyomo ndani ya documentary hii iko tofauti na itamgusa kila mmoja," Roma alisema. 

Mwaka huu Roma alipata kunyakua tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards akiwa Mwanamuziki Bora wa Hip Hop na wimbo wake wa Mathematics kuchukua tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment