Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Thursday, June 14, 2012

DOGO JANJA AFURUSHWA NA MADEE

DOGO JANJA
DOGO JANJA ARUDI KWAO ARUSHA BAADA YA KUKOSANA NA MADEE.


Msanii Madee wa Tip Top Connection ambae ndio alikabidhiwa na wazazi kumlea na kumsimamia Dogo Janja azungumzia sababu zake za kumrudisha Dogo Janja mikononi mwa wazazi wake.

Madee asema ameshindwa kuishi na Dogo Janja.

Madee asema Dogo Janja aliekua form II katika shule ya Makongo High School amekataa kusoma na hawezi kukaa nae wakati hataki kusoma.

Madee afichua kuwa juzi alkua safarini Iringa na Mbeya na aliporudi mwalimu wa Dogo Janja limpigia simu na kumpa pole kwa sababu Dogo Janja anaumwa. Hata hivyo alipofika nyumbani akampata Dogo Janja akiwa mzima wa afya lakini kakataa kwenda shule na kudaganya ni mgonjwa.

DOGO JANJA AKIWA STENDI YA BASI ASUBUHI YA LEO
Baada ya malumbano, akamuuliza ka anataka kusoma au kuzurura mtaani? Dogo akajibu kwamba anataka kwenda kusoma kwaoArusha badala ya sas Dar Es Salaam, ikabidi ampigie simu baba yake palepale ambapo mzee wake aligahiri na kumuomba Madee asimrudishe Arusha  bali aendelee kukaa nae Dar.

Hata hivyo baadaye Madee alichukua simu ya dogo na akagundua vitu vingi sana vya kishenzi shenzi vilvyoandikwa kumhusu. Baada ya malumbano zaidi Dogo akakita palepale anataka kurdi Arusha na Madee akampa baraka zote.
DOGO JANJA NDANI YA BASI


Dogo kaondoka leo Asubuhi kuelekea kwao Arusha….. Swali je twajifunza nini hapa?
Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™. 9AM - 1PM      (MON - FRI)

No comments:

Post a Comment