Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Tuesday, May 1, 2012

KITABU: CHUO KIKUU CHA HIPHOP




KITABU: CHUO KIKUU CHA HIPHOP
Hiki ni kitabu kuhusu Hip Hop kimeandikwa na M.S. HANZI "MALLE" ni mwanafunzi wa Chuo Cha Ustawi wa jamii Dar es salaam nchini Tz.

Dhumuni la kuandika kitabu hiki ni kutoa mwanga kwa jamii kuhusu Hip Hop na ukweli uliopo kuondoa mtazamo hasi kwamba Hip Hop ni uhuni, ni ya rika fulani tu, kutokana na makosa maarifa utamaduni wa Hip Hop, vijana wengi duniani wanakosea kwa kufikiri vitu/vitendo kama kuvuta bangi, kunywa vileo, kuvaa mavazi ya wabunifu, kujibandika plasta zenye alama za x, kubeba bastola (gun) au kwenda kujirusha club ndo "Hip Hop" .

Hip Hop inafanywa kimakosa sana na wasanii wengi ambao wanafanya kazi katika nguzo ya ughanaji (uchenguaji). 

Na haya makosa yote kwa kawaida huhamasishwa na kupewa promo na kiwanda cha muziki na washirika wengine ambao hudumaza utamaduni huu kwa kuteka ufahamu wa vijana na maadili yao. 


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment