Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Tuesday, May 1, 2012

MWANAMKE MWENYE PHD YA HIPHOP




Dkt. Shani Omari
Licha ya kuwa muziki wa bongo fleva/Hip hop bado umekuwa hautiliwi maanani kama unaoweza kuleta mabadiliko katika jamii, baadhi ya wasomi wameanza kuifuta dhana hiyo.

Mmoja ya watu walioamua kuchukua hatua hiyo muhimu kwa maendeleo ya muziki huo, ni mwanadada Dkt. Shani Omari ambaye ametunukiwa shahada ya udaktari wa muziki wa hip-hop (PHD) mwaka 2009, katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuwa mwanamke na muhitimu wa kwanza hapa nchini kutunukiwa shahada hiyo.

Dk. Shani alipata mwamko wa kusomea Shahada hiyo, baada ya kuona muziki huo unadharauliwa licha ya kujulikana sana duniani.

Anasema uamuzi wa kuusomea zaidi muziki huo ulitokana na kuwa na mapenzi nao tangu akiwa mwanafunzi, hasa alipokuwa akisoma sekondari huku akipenda zaidi muziki wa kufokafoka ‘rap’ kuliko mitindo mingine, hususan michanio ya lugha ya Kifaransa.

Dk. Shani alizaliwa jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 1970 na kupata elimu ya msingi katika shule ya Kurasini mwa 1981- 1987, 1988-1991 akasoma sekondari ya Kibasila na 1992-1994 alisoma kidato cha tano na sita katika sekondari ya Zanaki.

Anawashauri wasanii kutambua kuwa wana nafasi kubwa ya kuielemisha na kuifunza jamii kupitia muziki, si katika kuimba tu bali pia kushirikiana na wadau mbalimbali na si mapromota na watayarishaji wa muziki tu.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

No comments:

Post a Comment