Mwana
mziki wa Bongo flava AY jumapili ya wikendi hii inayokuja anataajiwa kuvunja
rekodi na kuwa mtanzania wa kwanza kuperform kwa mara ya pili kwenye stage ya
Big Brother Africa.
Akizungumzia
matayarisho yake AY afichua pia kuna uwezekano akaitumia fursa hiyo kufanya
video yake pili.
Ni
wiki mbili zimepita toka atoke Afrika Kusini alikokwenda kufanya video yake ya
kwanza iliyomgharimu KSH milioni 3 iliyofanya na kampuni ya Godfather, ambayo
imefanya video nyingi za P Square, J Martins, Mr Flavour na wengine.
Akizungumzia
hatua yake ya kutumia fedha nyingi kwa video zake, AY asema “hii ni biashara na
biashara yoyote ni lazima uwekeze hakuna faida inayokuja tu bure bure, watu ni
uoga tu ujue wa kuwekeza wanabaki kuelekeza vidole kwa Wanigeria ambao
wanawekeza pesa kwenye muziki, mimi najibana pia ninachokipata nakigawa.. hata
zamani ilikua hivi hivi tu watu walikua wanashangaa Ay unakwenda Uganda
unapoteza hela, leo hii wao wanahangaika kwenda Uganda na Kenya mimi
nimeshatoka huko”
AY
anatarajiwa kuondoka bongo jumamosi hii kwenda nchini afrika kusini kuperform
katika show ya Big Brother siku ya jumapili akipanda stage moja na wakali wetu
wa Kenya Sauti Sol.
Kwa
mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" -
"Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu
Cha Umoja Wa Pwani ™. 9AM - 1PM (MON - FRI)
No comments:
Post a Comment