Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Monday, June 18, 2012

WASANII KULIPA USHURU:



HUENDA WASANII WAKAANZA KULIPA USHURU:
Huenda wasanii nchini wakaanza kulipa ushuru iwapo pendekezo la waziri wa feedha nchini Robinson Githae litaratibishwa na kuwa sheria nchini.

Katika bajeti yae wiki iliyopita waziri huyu alipendekeza wasanii wano piga show kulipa asilimia 16 ya ushuru kutoka kwa hela wanazopata wanapo tumbuiza watu katika mikahawa mbali mbali.

Haya yanajiri huku wasnii nchinikenya wakiendelea kutia kibindoni hela zote wanazo lipwa kufuatia ukosefu wa sheria ya kuhakikisha wanalipa ushuru kama wafanyavyo wasnii katika mataifa mengine.

Hivi karibuni msanii R. Kelly nchini Marekani amejipata matatani  baada ya kugunduliwa kwamba hajakuwa akilipa ushuru kama inavyotakikana kwa miaka mingi.

Je wasanii wetu Mombasani wakotayari kulipa ushuru?

Je,  hela wanazopata katika mashow zinastahili kukatwa ushuru?

Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza"Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.               9AM - 1PM      (MON - FRI)

No comments:

Post a Comment