Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Thursday, July 26, 2012

Z ANTO AJENGA NYUMBA MBILI

Z ANTO
Msanii wa mziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Z Anto afichua kuwa amejenga nyumba mbili kutokana na mapato yake ya kimziki.

Akifichua haya, Z Anto asema moja ya nyumba hizo imemgharimu kiwango kisichopungua milioni 45 hela za Tanzania, ambazo ni sawia na shilingi 250,000/=

Z Anto asema kwa sasa nyumba hiyo imekamilika na ameipangisha, huku akiendelea na ujenzi wa nyumba ya pili.

Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.9AM - PM. MON-FRI


LINEX NI MKULIMA

LINEX
 Mbali na kufanya mziki, msanii wa bongo flava nchni Tanzania maarufu kwa jina Linex afichua kua yeye ni mkulima.

Msanii huyu asema kuwa, yeye huendeleza kilimo cha vitunguu na karoti.

Linex afichua kuwa anaendeleza shughuli zake za ukilima katika sehemu ya Kigoma nchini Tanzania.

Akizungumzia faida za shughuli zake za ukilima Linex afichua kuwa alianza na mtaji wa shilingi milioni 3 za Tanzania amabazo ni sawa na shilingi166,000/= hela za Kenya.

Kwa sasa Linex asema biashara yake ya ukulima inaingiza faida ya milioni 7 hela za Tanzania ambazo ni sawa na shilingi 388,000/= hela za Kenya.


Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.9AM - PM. MON-FRI

Friday, July 20, 2012

JUA CALI SAVES A PLANE FROM CRASHING


JUA CALI
While on a recent European tour, Juacali became a local hero in Amsterdam after preventing a plane from crashing just before it took off. Here's what happened:

Juacali had just boarded a plane that was going from Amsterdam to London. He got the window seat. Looking outside as he sat in his chair, he noticed the left engine of the plane was producing some black smoke. Juacali sensed that something was amiss. He immediately alerted the beautiful air hostesses to the problem. Shortly afterwards, everybody was instructed to get off the plane.

The pilots said they were 5 minutes away from taking off but Jua Cali's keen observation actually saved the day. The airport paid for his trip and he was awarded with 10 bonus first class tickets, valid for 5 years.



For more information tune to Kaya Flavaz on RadioKaya 93.1Fm Msa 99.7Fm Mlnd every Mon - Fri from 9am to get the best of coast urban music.

Sunday, July 15, 2012

SIZE 8 NA HUSSEIN MACHOZI NI WACHUMBA?


SIZE 8 & HUSSEIN MACHOZI
SIZE 8 NA HUSSEIN MACHOZI NI WACHUMBA?
Uvumi unadai kuwa sababu kuu iliyomfanya mwanamziki wa bongo Flava Hussein Machozi kuhamia Kenya ni kipusa mwanamziki wa hapa nchini Linet aka Size 8.

Hussein anadai amepata mwanamke aliyekuwa akimtafuta kwa mda mrefu maishani mwake na simwengine bali kipusa huyu aliyeteka taifa na kibao chake “Nawapa Vidonge”.

Hussein akana madai kwamba ameolewa na Size 8 na kufichua hivi karibuni atampeleka kwao Singida, Manyoni Tanzania akamtambulishe kwa wazazi wake.

Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.9AM - PM. MON-FRI


Wednesday, June 20, 2012

DIAMOND ANUNUA GARI LA KSH 3.1 MILLION

DIAMOND PLATINUMZ
DIAMOND ANUNUA GARI JIPYA:
Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini Tz kwa sasa anayepeta zaidi Naseeb Abdul ‘Diamond  Platinumz’ amenunua gari jipya lenye thamani ya shilingi milioni 3.1 pesa za Kenya ama za Tsh 60,00000(milioni 60)

Gari hilo ni aina ya Land Cruiser Prado TX 2006 na alilipokea rasmi kutoka kwa wakala aliyekuwa akishughulikia mpango mzima  wa  kuliingiza Bongo.
LAND CRUISER PRADO TX 2006
Akifichua hayo mda mfupi baada ya kupokea  gari hilo Diamond asema amekua na mipango ya kumiliki gari design hiyo lakini kulikua na mambo kadhaa ambayo alkua anapanga kukamilisha kabla ya kununua gari hilo.

Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.9AM - PM. MON-FRI



Monday, June 18, 2012

WASANII KULIPA USHURU:



HUENDA WASANII WAKAANZA KULIPA USHURU:
Huenda wasanii nchini wakaanza kulipa ushuru iwapo pendekezo la waziri wa feedha nchini Robinson Githae litaratibishwa na kuwa sheria nchini.

Katika bajeti yae wiki iliyopita waziri huyu alipendekeza wasanii wano piga show kulipa asilimia 16 ya ushuru kutoka kwa hela wanazopata wanapo tumbuiza watu katika mikahawa mbali mbali.

Haya yanajiri huku wasnii nchinikenya wakiendelea kutia kibindoni hela zote wanazo lipwa kufuatia ukosefu wa sheria ya kuhakikisha wanalipa ushuru kama wafanyavyo wasnii katika mataifa mengine.

Hivi karibuni msanii R. Kelly nchini Marekani amejipata matatani  baada ya kugunduliwa kwamba hajakuwa akilipa ushuru kama inavyotakikana kwa miaka mingi.

Je wasanii wetu Mombasani wakotayari kulipa ushuru?

Je,  hela wanazopata katika mashow zinastahili kukatwa ushuru?

Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza"Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.               9AM - 1PM      (MON - FRI)