Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Monday, April 30, 2012

FASH P AACHILIA WIMBO MPYA




FASH P 
FASH P AACHILIA WIMBO MPYA
Majina yangu kamili naitwa Benjamin Thoya Baya na nilizaliwa mwaka wa 1989 tarehe 5 mwezi wa kwanza.


Mimi ni msanii kutoka Malindi na nilianza mziki mnamo mwaka wa 2007 baada ya kumaliza masomo yangu ya sekondari.UKABILA ndio ngoma yangu latest ambayo nimemshirikisha msanii wa kike Baby Moe.Ngoma Hii imefanywa chini ya mkono wa producer Jay Crak wa Crack Sound Records (KILIFI)

Mbali na usanii mimi pia ni muigizaji na pia nasomea ualimu katika chuo cha ST Marks TTC Kigari kilichoko Embu.Katika mashindano yaliyojumuisha Vyuo vya ualimu vya eastern province ya drama, mimi niliibuka kama muigizaji bora wa pili wa tamasha hiyo.



Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.


DOWNLOAD: FASH P - UKABILA

Tuesday, April 24, 2012

BI. CHEKA AITWA MCHAWI

                  
BI. CHEKA AWAHI KUITWA MCHAWI.
Ajuza ambaye kwa sasa anapeta sana katika mziki wa kizazi kipya nchini Tanzania baada ya kufanya wimbo na Mh. Temba wa kundi la TMK, Bi. Cheka afichua kuwa kabla ya umaarufu wake wa kimziki aliwahi kuitwa mchawi.

Bi. Cheka asema kabla ya kuanza usaniii aliwahi kufanya biashara ndogo ndogo ikiwemo kuuza mahari mataani ambapo baadhi ya majirani wake walimvumisha kuwa mshirikina aka mchawi kufuatia uzee wake.

Bi. Cheka hata hivyo hajachelea kuwasamehe majirani wake ambao kwa sasa wameanza kubadilisha mitazamo yao kumhusu baada ya kupata mafanikio katika ulimwengu wa Bongo fleva.
        

Hata hivyo Bi. Cheka pia awanyoshea kidole cha lawama adui zake mtaani ambao bado hawajafurahishwa na hatua yake ya kimafanikio katika ulimwengu wa kimziki, kufuatia kile alichokitaja kama ugonjwa usiojulikana sababu yake ambao uliokumba wiki iliyopita.

Bi. Cheka adai ilibidi kupata matibabu kutoka kwa babu mmoja aliyempa miti shamba kuweza kumponya ugonjwa huo ambao hadi sasa haujabainika chanzo chake.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Sunday, April 15, 2012

KILIMANJARO AWARDS 2012 - TZ



WASHINDI KATIKA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2012

1. Best Reggae Song – ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST
2. Best Dance Hall Song – MANENO MANENO BY QUEEN DARLEEN
3. Best Zouk Rhumba song – DUSHELELE BY ALI KIBA
4. Best Traditional Song – VIFUU UTUNDU BY AT
5. Best Taarab Song – NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC (ISHA MASHAUZI)
6. Best Kiswahili Song – DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA
7. Best Afro Pop Song – HAKUNAGA BY SUMA LEE
8. Best R&B Song – MY NUMBER ONE FAN BY BEN POL
9. Best Hip Hop Song – MATHEMATICS BY ROMA
10. Best Upcoming Artist – OMMY DIMPOZ
11. Best Rapper from a Band – KALIJO KITOKOLOLO
12. Best Hip Hop Artist – ROMA MKATOLIKI
13. Best Collabo – NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA
14. Best East African Song – KIGEUGEU BY JAGUAR
15. Best Female Performer – KHADIJA KOPA
16. Best Composer – DIAMOND
17. Best Male Performer – DIAMOND
18. Best Producer – MANEKE (AM RECORDS)
19. Best Video – MAWAZO BY DIAMOND
20. Song of the Year – HAKUNAGA BY SUMA LEE
21. Hall of Fame to an Institution – JKT TAARAB
22. Hall of Fame to an Individual – KING KIKII
23. Hall of Fame to an Individual – DR. REMMY MTORO ONGALA
24. Best Female Singer – LADY JAY DEE
25. Best Male Singer – BARNABA






















Tuesday, April 10, 2012

ALI KIBA KUTUZWA NA PRODUCER




ALI KIBA

PRODUCER MAN WATER KUMTUZA ALI KIBA.
Producer Man Water wa studio ya Combination Sounds nchini Tanzania, ameendelea na mpango wake wa kuwatuza wasanii mbalimbali waliorekodi ndani ya studio yake na nyimbo zao kufanya vizuri katka ulimwengu wa Bongo Fleva.


Kwa mujibu wa Man Water, mwaka huu atawatuza wa wasanii wawili Ally Kiba pamoja na msanii mwengine anayejulikana kwa jina Mbatizaji.


Man Water asema lengo la kufanya hivyo ni kutoa shukrani kwa wasanii, ambao kwa namna moja ama nyingine wameitangaza vyema studio yake na kumfanya yeye mwenyewe kuweza kujulikana na kupata kazi nyingi zaidi.


Alisema awali aliianza kwa msanii 20% na kumpa zawadi ya baadhi ya vyombo vya muziki na hivyo kwa mwaka huu yupo mbioni kumtunuku Ally Kiba ambaye wimbo wake kwa jina 'Dushelele' aliourekodi katika studio yake ya Combination Sounds imeweza kukubalika vilivyo na mashabiki wa muziki ndani na nje ya Tanzania.


“Kiba ni msanii mzuri na ni kati ya wanaoweza kuufanya muziki huu kuwa bora zaidi na kututangaza nje ya mipaka yetu kwa urahisi zaidi…..naamini nitaendelea kufanya kazi naye ili kuweza kutengeneza nyimbo zenye ubora zaidi na kuwaelimisha na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya,” alisema.
Akimzungumzia Mbatizaji, Water alisema atamtunuku msanii huyo kutokana na wimbo wake wa ‘Heshima ya Kazi’ kuweza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga, akisema ni mmoja kati ya wasanii wenye tungo zenye maadili na kufundisha jamii.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Tuesday, April 3, 2012

ONE OF THE BEST HIPHOP LOVE SONGS FROM CHIDI BENZ


SUDIBOY AACHILIA WIMBO MPYA

SUDIBOY
SUDIBOY AACHILIA WIMBO MPYA KWA JINA " ACHIA NGAZI"


Msanii wa mziki wa Mombasani SUDIBOY aachilia wimbo mpya baada ya kimya cha mda mrefu.


Akizungumza na KAYA FLAVAZ, SUDIBOY ambaye kwa sasa anatamba na "collabo" aliyofanya na msanii mwengine wa Mombasani kwa jina ROJO kwa jina VAMPIRE, asema kuwa anaimani kazi yake mpya itamletea mafanikio ya kimziki.


SUDIBOY afichua kuwa wimbo wake mpya unajulikana kama ACHIA NGAZI na amemshirikisha msanii mwengine wa mziki wa Mombasani CHIKUZEE.



Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

DOWNLOAD: SUDIBOY&CHIKUZEE - ACHIA NGAZI

SHETTA KUACHILIA WIMBO MPYA



SHETTA


SHETTA KUACHILIA WIMBO BAADA YA PASAKA


Msanii wa Bongo Flavaz anayetamba na nyimbo "Nimechokwa" pamoja na "Mdananda", Shetta, afichua kuwa anapanga kuachilia wimbo mpya baada ya Sikukuu ya Pasaka.


Shetta asema wimbo huo unajulikana kwa jina ‘Nidanganye danganye’ . na kitu kimekalika ambapo mda mchache baada ya wimbo huo kutoka  mashabiki wake pia watapata kuiona video yake.


Hata hivyo msanii huyo alipoulizwa juu ya kutoa albamu kwa mwaka huu, alijibu kuwa “Naweza kutoa lakini kama unavyojua albamu hazima maslahi kabisa yani tunatoa basi tu,”.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

SULTAN WA PWANI AACHILIA SINGLE YAKE


SULTAN WA PWANI


NEW KID ON THE BLOCK

SULTAN WA PWANI ni Msanii kutoka Mombasani. His real names are ALI KOMBO born in coast

He had Interest for music since childhood but started composing songs in 2003.
Anasema he recorded two songs but hakufika mahali!!

Amefanya kazi na K-SHOT of Green House Records, N.J.E wa ufuoni rec.
In 2010 was when He mate producer Mobiz from thundersound records, and thats
where he signed at, he has worked with shirko the song was okoa maisha ..with various coast artist.


Pia he worked with Rojo-mo on track by the title "Cheza Ngoma", Chikuzee na pia Sudi Boy the song: ZIKI LA NAZI which is yet to be released and was recorded by amz at S.Q records.

And now he has done his first Solo track titled SITAKI KERO.

DOWNLOAD: SULTAN WA PWANI - STAKI KERO

His personal number: 0715523986.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.