Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Monday, May 7, 2012

ROMA KUTOA "DOCUMENTARY" YA MAISHA YAKE.


ROMA 
Mwanahiphop bora kwa mwaka 2012, Ibrahim Mussa maarufu kama Roma Mkatoliki ako katika harakati za kutengeneza documentary”  itakayoelezea maisha yake ya mziki tangu alipoanza hadi alipofikia sasa. 

Roma ambaye anatamba na kibao Mathematics asema kuwa documentary hiyo itaweka wazi maisha yake aliyoyapitia pamoja na vikwazo alivyovipitia. 

"DVD hii inatengenezewa hapa katika studio za Tongwe Records na ni mapema sana kusema kuwa itatoka lini ila haitochelewa kutoka na naamini watu wataipenda na italeta utofauti kidogo maana story iliyomo ndani ya documentary hii iko tofauti na itamgusa kila mmoja," Roma alisema. 

Mwaka huu Roma alipata kunyakua tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards akiwa Mwanamuziki Bora wa Hip Hop na wimbo wake wa Mathematics kuchukua tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Thursday, May 3, 2012

CHIDI BENZ AZUNGUMZIA KUTOBOA PUA




“NIMETOBOA PUA KUONYESHA HISIA” - CHIDI.

Msanii wa Hiphop Bongo flava kwa Rashid Jumanne a.k.a CHID BENZ amezua hisia tofauti miongoni mwa wakereketwa wa mziki wa Bongo Flava hususan wanaume baada ya kuamua kutoba pua yake.

Hata hivyo akizungumzia hatua aliyochokua, kiongozi huyo wa kundi la 'LA FAMILIA' lenye maskani yake Ilala jijini Dar Es Salaam aeleza aliamua kutoboa pua (kutoga) ili kuonyesha hisia za maumivu aliyoyapata miaka iliyopita. 
CHID BENZ asema kwa muda amekua akiumizwa katika nyanja za mapenzi, safu nyenginezo na aliona bora atoboe pua ili apate maumivu, ambayo kwake itabakia kuwa kumbukumbu.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Wednesday, May 2, 2012

DIAMOND AWEKA HISTORIA UKUMBI WA DAR LIVE!

                                                DIAMOND AWEKA HISTORIA
Diamond tayari kupanda Chopper

Diamond akiwa na Rubani wake wakielekea kwenye chopper
Akitoa saluti kabla ya kupasua anga.
Akipiga sala kabla ya chopper kupaa hewani
Chopper ikaribia kutua

Kiota cha burudani cha DarLive kwa muonekano wa juu, maelfu ya mashabiki wakishubiri raisi wa wasafi atue

Akitoa saluti kwa rubani wake baada  ya kutua salama.

DarLive ikiwa full.

Diamond Platnumz akiwa kwa stage












Tuesday, May 1, 2012

RICH ONE ATAPELI MAPROMOTA AKIJIITA "ALI KIBA"



RICH ONE KITUO CHA POLISI

Aliyewahi kuwa member wa kundi la TMK Wanaume Halisi Rich One, anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Msimbazi kwa kosa la kutumia jina la Ali Kiba kuwatapeli mapromota mbali mbali.

Msanii huyo anadaiwa ku-divert simu zinazopigwa kwa namba ya Ali Kiba na kuzipeleka katika simu yake, baada ya hapo anakubaliana na mapromota kufanya show na kupokea advance kwa kuwapa namba yake ya mpesa. Siku ya show promota anajikuta katika wakati mgumu baada ya kutokumuona Ali Kiba.
Meneja wa Ali Kiba, Frank Gonga amethibisha kukamatwa kwa Rich One.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

MWANAMKE MWENYE PHD YA HIPHOP




Dkt. Shani Omari
Licha ya kuwa muziki wa bongo fleva/Hip hop bado umekuwa hautiliwi maanani kama unaoweza kuleta mabadiliko katika jamii, baadhi ya wasomi wameanza kuifuta dhana hiyo.

Mmoja ya watu walioamua kuchukua hatua hiyo muhimu kwa maendeleo ya muziki huo, ni mwanadada Dkt. Shani Omari ambaye ametunukiwa shahada ya udaktari wa muziki wa hip-hop (PHD) mwaka 2009, katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuwa mwanamke na muhitimu wa kwanza hapa nchini kutunukiwa shahada hiyo.

Dk. Shani alipata mwamko wa kusomea Shahada hiyo, baada ya kuona muziki huo unadharauliwa licha ya kujulikana sana duniani.

Anasema uamuzi wa kuusomea zaidi muziki huo ulitokana na kuwa na mapenzi nao tangu akiwa mwanafunzi, hasa alipokuwa akisoma sekondari huku akipenda zaidi muziki wa kufokafoka ‘rap’ kuliko mitindo mingine, hususan michanio ya lugha ya Kifaransa.

Dk. Shani alizaliwa jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 1970 na kupata elimu ya msingi katika shule ya Kurasini mwa 1981- 1987, 1988-1991 akasoma sekondari ya Kibasila na 1992-1994 alisoma kidato cha tano na sita katika sekondari ya Zanaki.

Anawashauri wasanii kutambua kuwa wana nafasi kubwa ya kuielemisha na kuifunza jamii kupitia muziki, si katika kuimba tu bali pia kushirikiana na wadau mbalimbali na si mapromota na watayarishaji wa muziki tu.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

KITABU: CHUO KIKUU CHA HIPHOP




KITABU: CHUO KIKUU CHA HIPHOP
Hiki ni kitabu kuhusu Hip Hop kimeandikwa na M.S. HANZI "MALLE" ni mwanafunzi wa Chuo Cha Ustawi wa jamii Dar es salaam nchini Tz.

Dhumuni la kuandika kitabu hiki ni kutoa mwanga kwa jamii kuhusu Hip Hop na ukweli uliopo kuondoa mtazamo hasi kwamba Hip Hop ni uhuni, ni ya rika fulani tu, kutokana na makosa maarifa utamaduni wa Hip Hop, vijana wengi duniani wanakosea kwa kufikiri vitu/vitendo kama kuvuta bangi, kunywa vileo, kuvaa mavazi ya wabunifu, kujibandika plasta zenye alama za x, kubeba bastola (gun) au kwenda kujirusha club ndo "Hip Hop" .

Hip Hop inafanywa kimakosa sana na wasanii wengi ambao wanafanya kazi katika nguzo ya ughanaji (uchenguaji). 

Na haya makosa yote kwa kawaida huhamasishwa na kupewa promo na kiwanda cha muziki na washirika wengine ambao hudumaza utamaduni huu kwa kuteka ufahamu wa vijana na maadili yao. 


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.