BELLE9 - AMERUDI "VIDEO"
Kaya Flavaz
Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.
Wednesday, June 27, 2012
Wednesday, June 20, 2012
DIAMOND ANUNUA GARI LA KSH 3.1 MILLION
DIAMOND PLATINUMZ |
Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini Tz kwa sasa
anayepeta zaidi Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinumz’ amenunua gari jipya lenye thamani ya shilingi milioni 3.1
pesa za Kenya ama za Tsh 60,00000(milioni 60)
Gari hilo ni aina ya Land Cruiser Prado TX 2006 na
alilipokea rasmi kutoka kwa wakala aliyekuwa akishughulikia mpango mzima wa kuliingiza
Bongo.
LAND CRUISER PRADO TX 2006 |
Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani
Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.9AM - PM. MON-FRI
Monday, June 18, 2012
WASANII KULIPA USHURU:
HUENDA WASANII WAKAANZA KULIPA USHURU:
Huenda wasanii nchini wakaanza kulipa ushuru iwapo
pendekezo la waziri wa feedha nchini Robinson Githae litaratibishwa na kuwa
sheria nchini.
Katika bajeti yae wiki iliyopita waziri huyu
alipendekeza wasanii wano piga show kulipa asilimia 16 ya ushuru kutoka kwa
hela wanazopata wanapo tumbuiza watu katika mikahawa mbali mbali.
Haya yanajiri huku wasnii nchinikenya wakiendelea
kutia kibindoni hela zote wanazo lipwa kufuatia ukosefu wa sheria ya
kuhakikisha wanalipa ushuru kama wafanyavyo wasnii katika mataifa mengine.
Hivi karibuni msanii R. Kelly nchini Marekani
amejipata matatani baada ya kugunduliwa
kwamba hajakuwa akilipa ushuru kama inavyotakikana kwa miaka mingi.
Je wasanii wetu Mombasani wakotayari kulipa ushuru?
Je, hela
wanazopata katika mashow zinastahili kukatwa ushuru?
Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza"Show Nambari Moja Mkoani
Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd
- "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™. 9AM - 1PM
(MON - FRI)
OCTOPIZZO KUANZA BIASHARA YA CONDOM:
OCTOPIZZO ANAPANIA KUANZISHA “BRAND” YA CONDOM:
Msanii chipkizi jijini Nairobi anayetamba kwa sasa
kwa jina Octopizzo afichua kuwa anamipango ya ku’launch ‘brand’ yake ya aina ya
‘Condom’ nchini.
Katika mahojiano na kitupo kimoja cha TV jijini
Nairobi, Octopizzo asema ‘brand’ yake ya ‘condom’ itakua na ‘condom’ nne katika
‘Pack’ moja ‘instead ‘ya tatu kama ‘brand’ zegine za ‘condom’ nchini.(Duh!!!)
Hatua ya msanii huyu haitakuwa geni katika ulimwengu
wa mziki wa kizazi kipya, kwani kuna wasanii wakubwa ulimwenguni ambao
wameanzisha biashara ambazo haziambatani na mziki wao.
Mfano 50cent anakampuni ya maji ya ‘Vitamins’ huku
msanii kama ‘Jay Z’ mbali na nguo akimiliki hisa katika klabu ya ‘New York Mets’
ya mchezo wa vikapu nchini Marekani.
Je ndoto hizi zitatimia?
Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani
Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd -
"Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.
9AM - 1PM (MON - FRI)
Thursday, June 14, 2012
AY KUFANYA VIDEO MBILI KWA MILIONI 6 AFRIKA KUSINI
Mwana
mziki wa Bongo flava AY jumapili ya wikendi hii inayokuja anataajiwa kuvunja
rekodi na kuwa mtanzania wa kwanza kuperform kwa mara ya pili kwenye stage ya
Big Brother Africa.
Akizungumzia
matayarisho yake AY afichua pia kuna uwezekano akaitumia fursa hiyo kufanya
video yake pili.
Ni
wiki mbili zimepita toka atoke Afrika Kusini alikokwenda kufanya video yake ya
kwanza iliyomgharimu KSH milioni 3 iliyofanya na kampuni ya Godfather, ambayo
imefanya video nyingi za P Square, J Martins, Mr Flavour na wengine.
Akizungumzia
hatua yake ya kutumia fedha nyingi kwa video zake, AY asema “hii ni biashara na
biashara yoyote ni lazima uwekeze hakuna faida inayokuja tu bure bure, watu ni
uoga tu ujue wa kuwekeza wanabaki kuelekeza vidole kwa Wanigeria ambao
wanawekeza pesa kwenye muziki, mimi najibana pia ninachokipata nakigawa.. hata
zamani ilikua hivi hivi tu watu walikua wanashangaa Ay unakwenda Uganda
unapoteza hela, leo hii wao wanahangaika kwenda Uganda na Kenya mimi
nimeshatoka huko”
AY
anatarajiwa kuondoka bongo jumamosi hii kwenda nchini afrika kusini kuperform
katika show ya Big Brother siku ya jumapili akipanda stage moja na wakali wetu
wa Kenya Sauti Sol.
Kwa
mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" -
"Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu
Cha Umoja Wa Pwani ™. 9AM - 1PM (MON - FRI)
DRAKE APIGANA NA CHRIS BROWN
CHRIS BROWN |
Taarifa kutoka nchini Marekani zadai kuwa msanii kwa
jina Drake kutoka kundi la YMCMB amepigana na msanii wa mwengine wa RnB nchini
kwa jina Chris Brown.
DRAKE |
Taarifa hizo zadai wasanii hao walkutana katika
klabu moja usiku jiji New York . inadia msanii Chris Brown alinunua Champagne na kumtuma mmoja wa wahudumu wa klabu hiyo
kupelekea kinyaji hicho kwa meza ya akina Drake lakini msanii Drake akamua
kurudisha kinywaji hicho pamoja na ujumbbe katika kikaratasi ( “I’m F*******
the love of your life) akimaanisha msanii wa kike Rihanna.
Ghafla bin vu vuramai likazuka na jamaa hawa wawili
wakaamua kuzichapa kavu kavu bila gloves za boxing.
Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™. 9AM - 1PM (MON - FRI)
KIDEVU CHA CHRIS BROWN BAAD AYA VURUMAI |
DOGO JANJA AFURUSHWA NA MADEE
DOGO JANJA |
DOGO JANJA ARUDI KWAO ARUSHA BAADA YA KUKOSANA NA MADEE.
Msanii Madee wa Tip Top Connection ambae ndio alikabidhiwa na wazazi kumlea na kumsimamia Dogo Janja azungumzia sababu zake za kumrudisha Dogo Janja mikononi mwa wazazi wake.
Msanii Madee wa Tip Top Connection ambae ndio alikabidhiwa na wazazi kumlea na kumsimamia Dogo Janja azungumzia sababu zake za kumrudisha Dogo Janja mikononi mwa wazazi wake.
Madee asema ameshindwa kuishi na
Dogo Janja.
Madee asema Dogo
Janja aliekua form II katika shule ya Makongo High School amekataa
kusoma na hawezi kukaa nae wakati hataki kusoma.
Madee afichua kuwa juzi alkua
safarini Iringa na Mbeya na aliporudi mwalimu wa Dogo Janja limpigia simu na
kumpa pole kwa sababu Dogo Janja anaumwa. Hata hivyo alipofika nyumbani akampata
Dogo Janja akiwa mzima wa afya lakini kakataa kwenda shule na kudaganya ni
mgonjwa.
DOGO JANJA AKIWA STENDI YA BASI ASUBUHI YA LEO |
Baada ya malumbano, akamuuliza ka anataka kusoma au kuzurura mtaani? Dogo akajibu kwamba anataka kwenda kusoma kwaoArusha badala ya sas Dar Es Salaam, ikabidi ampigie simu baba yake palepale ambapo mzee wake aligahiri na kumuomba Madee asimrudishe Arusha bali aendelee kukaa nae Dar.
Hata hivyo baadaye
Madee alichukua simu ya dogo na akagundua vitu vingi sana vya kishenzi shenzi vilvyoandikwa
kumhusu. Baada ya malumbano zaidi Dogo akakita palepale anataka kurdi Arusha
na Madee akampa baraka zote.
DOGO JANJA NDANI YA BASI Dogo kaondoka leo Asubuhi kuelekea kwao Arusha….. Swali je twajifunza nini hapa? |
Kwa mengi Zaidi usikose kuskiza "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™. 9AM - 1PM (MON - FRI)
Subscribe to:
Posts (Atom)