Kaya Flavaz

Kwa Uhondo Wa Habari Za Sanaa Ya Mombasani.

Wednesday, February 29, 2012

AVRIL AFICHUA UGUMU WA KUANDIKA NYIMBO YAKE MPYA



AVRIL

AVRIL AFICHUA UGUMU WA KUANDIKA “ KITU KIMOJA”

Mwimbaji Avril afichua kwamba idea ya kwanza ya melody ya wimbo wake mpya “Kitu kimoja” ilikataliwa na producer wake Lucas wa Ogopa DJ’S.

Avril asema Lucas alimpa challenge afanye wimbo mzuri kuhusu mapenzi na kumtaka amuandikie wimbo mtu asie na uwezo wa kuona.

Avril  asema Lucas alitaka wimbo atakao uandika umfanye kipofu afurahi na ajisikie kupendwa.

“Nilijaribu kuhepa hepa hii idea akaniambia hapana rudi hukuuuuu”

Avril ambaye ameanza ujenzi wa nyumba ya wazazi wake akitumia pesa za faida ya mziki wake, amesema “ili kupata idea ya kuandika huu wimbo ilinibidi nifunge macho na kuaanza kuiandika na maneno yakawa yanakuja tu”

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Sunday, February 26, 2012

MSANII WA MALINDI KLEANHEART ATOA WIMBO MPYA





KLEANHEART

Emmanuel Ogutu a.k.a Kleanheart ni msanii wa Hip Hop na R&B kutoka mji wa  Malindi {Chocolate City} ambaye alianza safari yake ya mziki mwaka wa 1997 akiwa katika kikosi cha “Akraba” wakiwemo na wasanii wengine “Jix” na “Mc Diddy.”

Amekuwa nyuma ya pazia ya muziki huku mashabiki wake wakiwa na hamu yakutakakujuwa chanzo cha kimya chake. Akifichua sababu yenyewe Kleanheart asme masomo yalikosa kumpa nafasi ya kushughulikia mziki hadi pale alipo maliza kidato cha nne mwaka wa 2006.

Ni mzaliwa wa mji wa Malindi Kisumu-Ndogo na alisomea shule ya msingi ya Malindi Primary school(HGM) kabla ya kupata elimu ya upili Kakuyuni Secondary. Hajaoa yupo “single” na ni mtoto wa tisa katika family ya Mama Nora Ogutu na Mzee Ogutu Atata babake ,ambaye ni marehemu kwa sasa.

Hali yake kama Mlemavu ni changamoto pia katika maisha yake ya kisanii japo ndoto zake ni kubwa na zinamuacha na matumaini mengi. Klean heart alidondosha vibao kama “Tabia za madem”, “Naitwa pesa,” “Nipe nafasi” na pia kushirikishwa katika kolabo mbalimbali kama “Take it slow,” aliyoifanya na msanii GRA, “Marina” ya msanii Musha, “Joy” ya msanii  Escobar miongoni mwa nyenginezo.

Ni mmiliki mkuu wa Heartland Films kampuni inayo shughulika na filamu na video za muziki mjini Malindi. Pia anahusika na utayarishi wa gazeti la kila mwezi ambalo karibu litakuwa nje kwa jina MTAZAMO MAGAZINE. 

Kwa sasa Kleanheart ametoa wimbo mpya kwa jina "CHEMCHEM ZA KISANII " ajia kutoka kwa albam yake ya pili kwa jina “AKILI KICHWANI".

Anawaomba mashabiki wamshike mkono katika safari ndefu ya muziki huku akiwaahidi mambo mapya kila uchao.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Friday, February 24, 2012

MR. BLUE KUBADILI STYLE YA MZIKI


Mr. Blue
MR. ARUDIA STYLE YAKE YA KUIMBA.

Msanii wa Bongo Flava Mr. Blue a.k.a Byser, afichua kuwa anajaribu kubadilisha style ya muziki anayofanya kutoka kuimba hadi kurap.

Mr. Blue asema anatamani sana kurudi kwenye style yake ya zamani ambayo ndio iliyomtoa katika  ulimwengu wa muziki.

Kusistiza hatua yake Mr.  Blue afichua kuwa hivi karibuni atakua ana’release wimbo mpya ambao utaweka wazi style yake mpya.

 “Sihitaji kuimba kwa sasa kwa sababu najua style ambayo awali iliniweka juu kwenye chart, mashabiki wangu wataona utofauti wangu katika ngoma mpya ambayo itakuwa hewani soon,” alisema.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Thursday, February 23, 2012

TUNAMKUMBUKA NA KUMUENZI SIR MALCOM P



Sir Malcom P
R.I.P SIR MALCOM P

Wakereketwa wa mziki Mombasani leo waadhimisha miaka miwili tangu kuondoka kwa msanii maarufu katika ukanda wa pwani Sir Malcom P.

Malcom P ambaye majina yake halisi ni Malcom Puga, alifariki siku kama ya leo mwaka wa 2010 kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika barabara kuu ya Likoni - Lungalunga










Marehemu alikua ametoka nyumbani kwake Ukunda akielekea Kaloleni katika mkahawa mpya wa Kings ambako alikua anaenda kusherekea siku ya kuzaliwa kwake na alikuwa anafikisha miaka 35

Malcom P alikuwa meneja wa wa klabu ya Kings – Ukunda na Kings Recording studio na alikuwa amaefungua mkahawa mpya njini Kaloleni uliokuwa pia unaitwa Kings – Kaloleni.













Jumatano ya tarehe 24.02.2010 daima itabaki katika kumbukumbu za wakereketwa wa game ya Mombasani, kwani ni siku waliyompoteza kigogo wa game aliyekuwa ameshika mikono na kuwaenua wasanii na maproducer mbalimbali pwani, mbali na kufanya kazi zilizokubalika na wasanii wa taifa jirani la Tanzania.

Msanii Malcom P aliwahi kufanya kazi na kundi la TMK family, PNC na Yakuza Mobb.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

BABY MADAHA AJIUNGA TMK HALISI!



Baby Madaha


Mwanadada aliyeibukia kwenye shindano la Bongo Star Search, Baby Madaha, ajiunga rasmi na Kundi la TMK Wanaume Halisi linaongozwa na Juma Kassim Ally Kiroboro ‘Sir Nature’.

Akithibitisha, Baby Madaha asema kuwa mwaka huu ameamua kujipanga vyema zaidi ndiyo maana ameungana na TMK Wanaume Halisi.

Kwa upande wa Nature afichua kuwa kwa sasa Baby Madaha ndiye first lady wa kundi la TMK Wanaume Halisi.

“Tumemchukua kwa sababu anaweza kazi” alisema Juma  Nature.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Wednesday, February 22, 2012

MSANII ANAPO'HIT NANI WA KUPEWA SHUKRANI?



NANI ANAYEFAA KUPEWA SHUKRANI BAADA YA MSANII KU’HIT KATIKA INDUSTRY?

Msanii hupitia safari ndefu, akipitia mikononi mwa washikadau mbali mbali katika sekta ya sanaa kabla ya ku’hit. Hata hivyo baada ya msanii kuafikia ndoto yake ya kupata umaarufu na mafanikio ya kifedha katika ulimwengu wa mziki, nani anafaa kupewa shukrani kufuatia mchango wake mkubwa ama umuhimu mkubwa katika kufanikisha haya yote?

Wengi tuna majibu tofauti kufuatia mitazamo yetu tofauti lakini ningeomba mwanzo huyu msanii mwenyewe tumtoe katika orodha ya majibu yetu kwa sababu ni yeye tunamzungumzia kwa leo.
Pili mwenyezi mungu ambaye sote tunakubaliana kwamba ni mwezesha wa yote katika sanaa, mwanzo wa kila kitu na ambaye hatupingi uwezo wake.

Sekta ya sanaa hususan hapa Mombasani imetajwa kushirikisha washikadau mbalimbali ikiwemo ma’producer,ma’promoter,ma’presenter na wasikilizaji.  Washikadau hawa hutekeleza majukumu mbali mbali na kuchangia kwa usawa katika kukua kwa sanaa ya mziki. Hata hivyo wengi ya wasanii niliokumbana nao katika harakati za kusukumu gurudumu la sanaa wameniuliza swali hili, “je tutakapo hit nani tumshukuru zaidi?” Katika uchanganuzi wa washikadau katika jamii kupitia mchango wa waskilizaji tukufu wa kipindi cha “Chipkizi Za Kaya”, tunapata picha kamili ya majukumu mbali mbali ya washkadau wakuu katika sekta ya mziki wa Mombasani.

Producer hua mwanzo wa safari nzima ya msanii na huchangia pakubwa katika kuasisi mafanikio ya msanii yeyote. Wengi ya ma’producer wetu huwa wajuzi wa sanaa ya mziki mbali nakufahamu vyema jinsi ya kuruka viunzi tofauti tofauti katika mbio za kutafuta mafanikio ya kimziki. Katika kipindi cha “Chipkizi Za Kaya” ndani ya Radio Kaya jumapili ya tarehe 19, baadhi ya wasikilizaji waliotoa michango yao kuhusiana na mjadala huu walimtaja producer kama kiungo muhimu zaidi. Wengi walidai yeye ndio hupika chakula ambacho wao hutokea kukipenda. Wakimlenganisha na mpishi jikoni, wengi wahoji kuwa producer nyakati zozote hushikilia funguo ya ufanisi kwa msanii kwani yeye ndio ataamua kuongeza ama kupunguza chumvi katika chakula ambacho msikilizaji ataamua kama nikitamu ama hakifai.

Promoter pia atajwa katika orodha ya washikadau wakuu katika sekta ya mziki ambao pia huchangia pakubwa katika ufanisi wa msanii hususan limbukeni ama anayechipuka. Promoter anasemekana kuwa mfadhili wa ndoto nzima ya msanii. Kulingana mashabiki waliotoa mchango wao, promoter pia anaeza kulinganishwa na mjasiriamali kwani katika mchakato mzima wa kumfadhili msanii, hua analenga kufaidika baada ya msanii kufanikiwa kupitia pesa zitakazo kusanywa wakati wa ma’show. Kufuatia kutotaka kupoteza mtaji alioekeza katika msanii, promoter hufanya kila awezalo kuhakikisha msanii ana’hit katika industry. Pia wengi  washikilia kuwa promoter  hua katika stage muhimu ya usanii. Stage ya uasisi wa ndoto nzima. Bila yeye msanii huvunjika moyo na  wengine huachana na maswala ya mziki huku uwepo wa support yake humtia moyo msanii kufanya bidii. Katika pointi hii msikilizaji mmoja amfananisha promoter na mzazi kwa mwanafunzi, ambapo humlipia fees na kumuachia mwanafunzi jukumu la kutia bidii kufanikiwa.

Presenter tunazungumzia mtangazaji wa redio ambaye hucheza wimbo wa msanii na kumtambulisha kwa mshikadau mwengine ambaye ni msikilizaji. Wengi walisistiza ulazima katika kuwepo kwa uhusiano mwema kati ya mshikadau huyu na yule awali kwa jina promoter. Wasikilizaji wengi wadai uhusiano huu hua na mchango mkubwa katika jinsi msanii atakavyowasilishwa kwa maskio ya waskilizaji. Kazi ya presenter kitaaluma huhusisha kuskiliza kazi za msanii na kuamua iwapo zitawaburudisha wasikilizaji wake anapokua hewani. Jukumu hili alitwekwa baada ya kubainika kwamba kufuatia uzoefu wake katika kazi, anaweza kujua ni aina gani ya mziki msikilizaji wake hupenda. Baadhi ya waskilizaji waliochangia mjadala huu pia walihoji kuwa presenter hua na mamlaka ya kuamua kucheza ama kutocheza nyimbo. Jambo hili latajwa kumgeuza na kuwa wa muhimu zaidi katika mafanikio ya msanii. Swala la mshikadau huyu kuwa na uwezo wa kucheza ama kutocheza nyimbo hata anapoombwa na msikilizaji hewani latajwa kumpa uzito zaidi katika ratili ya mchakato huu.

Msikilizaji  ni yule anayeshabikia msanii katika redio. Mara nyingi hushirikiana kwa sana na presenter katika vipindi kabla ya kujiunga na mapromoter na msanii mwenyewe katika sehemu za burudani. Mara nyingi hupiga simu kuomba wimbo ama kuketi chini na kuskiza mziki unaochezwa katika kipindi. Kulingana na wengi waliochangia katika “Chipkizi Za Kaya” mshikadau huyu ni miongoni mwa wale wakuu katika game, kwani yeye ndiye anayetengenezewa nyimbo. Msanii anapo amua usanii lengo lake kubwa huwa ni kumrai na kumfurahisha msikilizaji. Promoter anapoamua kumfadhili msanii hulenga kufaidika baadaye msikilizaji huyu anapojitokeza katika sehemu za burudani kumwona msanii mwenyewe.

Presenter humtegemea sana mshikadau huyu kimaisha kwani yote anayofanya katika kazi yake hua ni kuhakikisha msikilizaji anafurahi na kuganda katika kipindi chake kila uchao. Kwa vile msikilizaji anaamua mwenyewe nyimbo gani inayo mfurahisha, presenter mara nyingi hana budi bali kucheza wimbo ule msikilizaji anaoufagilia zaidi. Katika muktadha huu, wengi ya walioshiriki mjadala huu walikubaliana kwamba shabiki  huamua  ni nyimbo gani inayo hit. Mskilizaji pia atajwa kuwafanya ma’promoter, ma’ presenter na ma’ producer kuwa busy kwani wote huwa katika harakati za kujaribu kumridhisha mshikadau huyu. Umuhimu wake watajwa kuongezeka zaidi pale anapopewa nafasi na presenter kuchagua wimbo utakaochezwa katika vipindi vya redioni.

Je nani anayefaa kupewa shukrani baada ya msanii ku’hit katika industry?



 (c)mwanamgambo2012



UJUMBE WA SUGU KWA WANAVINEGA BAADA YA MAPATANISHO





KWA WANAVINEGA:

KWANZA POLENI NA SAMAHANINI KWA HALI YA SINTOFAHAMU ILIYOTOKEA LEO KUTOKANA NA TAARIFA ZA GHAFLA ZA USULUHISHI KATI YETU NA RUGE/CLOUDS FM,NI KUTOKANA NA UNYETI WA ISSUE YENYEWE ILIBIDI TUFANYE HIVYO KWA NIA NJEMA KABISA...KWANZA NAOMBA TUJIPONGEZE KWA KUWA TUKIO LA LEO NI USHINDI KWA VINEGA KWA MAANA KWAMBA MADAI YETU YOTE YA MSINGI NDIO YALIKUWA MSINGI WA MAJADILIANO NA RUGE AMEKUBALI KUYATEKELEZA YOTE...

KUANZIA SUALA LA STUDIO YA RAIS KURUDISHWA KWA BASATA ILI IWE YA WASANII WOTE,PIA T.F.U IJIKABIDHI KWA CHAMA HALALI CHA WASANII YAANI T.U.M.A KAMA AMBAVYO TULIKUWA TUNADAI NA MPAKA ISSUE ZA WASANII KUNYANYASWA NA KUBANIWA NA PIA SUALA LA MALIPO HAFIFU VYOTE VIMEJADILIWA NA KUKUBALIWA KWA UTEKELEZAJI.HAIKUWA KAZI RAHISI,KWANZA ILIANZA KWA WAO KUMPIGIA MWENYEKITI WANGU MBOWE KUTAKA TUKAE CHINI,AMBAPO KAMANDA MBOWE ALINISHAURI TUKAE NAO CHINI KAMA KWELI WANA NIA YA KUYAMALIZA...BAADAYE WAKAMPIGIA MR SHIGONGO AMBAYE NI WAZI KUWA NI KATI YA WATU WANGU WA KARIBU NAYE BAADA YA KUONGEA NA MR. KUSAGA TU ALINIPIGIA NA KUNISHAURI HIVYO HIVYO.

NA KAMA HAIKUTOSHA WAKALIFIKISHA HILI SUALA KWENYE KAMATI YA BUNGE AMBAYO ILINITAKA NIIPE MAELEZO YA KIINI CHA MGOGORO NA NIKAFANYA HIVYO AMBAPO PIA BAADA YA KUNIELEWA WAKASHAURI NIKAE NAO CHINI...NA HATIMAYE SUALA HILI LIKAISHIA MIKONONI MWA WAZIRI NCHIMBI PAMOJA NA MHE. TUNDU LISSU(MP) KUWA WAPATANISHI WETU...WAZIRI NCHIMBI AKAANZA KWA KUMUITA RUGE DODOMA NA ALIKUJA TUKAKAA KWA HATUA YA KWANZA NA HATIMAYE LEO TUKAKAA TENA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA UTAMADUNI CHINI YA DR NCHIMBI NA MHE TUNDU LISSU NA HATIMAYE TUKAFIKIA HATUA HII YA LEO...VITA YETU ILIKUWA NA HOJA HATUKUWA TUNAPIGANA TU KWA CHUKI BINAFSI KAMA BAADHI YA WATU WALIVYOKUWA WANAJARIBU KUIWEKA,KWAHIYO KAMA HOJA ZETU ZIMEELEWEKA KWA SASA TUNATAKIWA KUSHUKURU NA KUFURAHIA...LAKINI NAOMBA NIWAHAKIKISHIE MISIMAMO IKO PALE PALE NA NIMEWAWEKA WAZI KUWA ANTI-VIRUS ITAENDELEA KUWEPO ILI KUENDELEA KU-SCAN VIRUS WENGINE KAMA MAMENEJA MASOKO NA WENGINE WATAKAOJITOKEZA KWANI NCHI INAPOSHINDA VITA AU HATA KUFIKIA TU MAKUBALIANO YA AMANI NA NCHI ADUI YAKE HAINA MAANA NCHI HIYO INAVUNJA JESHI LAKE...

ASANTENI SANA.
SUGU

Tuesday, February 21, 2012

BIFU YA MR. TWO NA CLOUDS FM - TZ YAFIKA KIKOMO



MR.  TWO NA MKURUGENZI WA CLOUDS FM WAPATANISHWA.

Hatimaye ugomvi wa Mkurugenzi wa Clouds Media (cloudsfmTz) Ruge Mutahaba na Mbunge wa jimbo la Mbeya kwa tiketi ya CHADEMA  Joseph Mbilinyi (Mr. Two Sugu) umemalizika baada ya kufanyika kwa vikao mbali mbali chini ya Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo wa Tanzania.
  

RUGE


Hatua hii yatia kikomo ugomvi wa maneno makali na bifu katika muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania uliopelekea kutochezwa kwa nyimbo za kundi la Vinega na kutolewa kwa album mbili za kuwapaka matope wafanyikazi mbali mbali wa Clouds Radio na Tv.

Baadhi ya wasanii wa Mombasani walikuwa wamejaribu kuiga bifu hii. Swali ni je kwa sasa watachukua hatua gani?

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

AMINI ATIMULIWA TANZANIA HOUSE OF TALENT



AMINI ACHUJWA KUTOKA JUMBA LA SANAA TANZANIA.


Siku chache baada ya kuripotiwa kwa msanii Amini kujadiliwa na uongozi wa THT Tanzania kufuatia madai ya utovu wa nidhamu, sasa imebainika kuwa msanii huyo ametimuliwa kutoka kwa THT.

Akithibitisha kutimuliwa kwake, Amini asema kuwa uongozi wa THT umemuonea na haujamtendea haki kutokana na mabavu yaliyotumika katika kujadili swala lake.

Amini asistiza hajafanya kosa na kufichua kuwa atafanya mziki kibinafsi.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Monday, February 20, 2012

CANNIBAL NA PREZZO KUJA MOMBASANI KUFANYA VIDEO:






“SCENES KADHAA ZA KATIKA VIDEO YA MY CITY MY TOWN ZITAKUWA ZA MOMBASA”

Msanii mkali wa mziki wa Mombasani Cannibal anakamailisha matayarisho ya ku’shoot video ya wimbo wake mpyao wa “My City my Town” aliomshirikisha msanii mkali wa Nairobi, Prezzo.

Akizungumza na Kaya Flavaz, Cannibal ambaye pamoja na Prezzo wanatengeneza kundi jipya la wanamziki nchini kwa jina MakiniMasaiMusic Group(MMMG) afichua kuwa, baadhi ya sehemu zitakazo tumiwa katika video hiyo zitakuwa jijini Mombasa hususan katika mistari inayotaja mkahawa wa Bellavista na hoteli ya Tarbush.

“Lazima kutakua na scenes za Mombasa kwa sababu huku Nairobi hakuna watoto wa kimanga wala wali wa nazi na biriani. Watu wa kujipaka hina wanapatikana Mombasani so itabidi tuje,” akasema.

Cannibal afichua kuwa atakuja Mombasa hivi karibuni ku’finalize kabla ya kurudi Nairobi na kushuka na mzee mzima Prezzo kwa shooting ya video.

Video shooting natumai itakua in the next two weeks lakini kabla hiyo time natarajia kuja Mombasa kukamilisha mipango kabla ya kurudi Nairobi halaf nishuke na Prezzo.

Cannibal pia afichua kuwa anapanga kufika Radiokaya kwa interview ndani ya show nambari moja mkoani pwani “Kaya Flavaz”.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Sunday, February 19, 2012

MASHANGINGI YASUMBUA WASANII WA BONGO.


YOUNG D, DOGO JANJA NA DOGO ASLAY WASUMBULIWA NA MAJIMAMA

Makinda wa Bongo Fleva, David Genz Mwanjela ‘Young D’, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ na Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ wadaiwa kusumbuliwa na mijimama kimapenzi huku baadhi yao wakidaiwa kuvuta bangi.

Baadhi ya wakereketwa wa sanaa ya Bongo Fleva  waomba wasani hawa wadogo wakatazwe mapema kujichanganya na tabia mbaya ambazo huenda zikahatarisha Maisha yao.

Msanii YOUNG D amabaye ana umri wa miaka 19 kwa sasa alikubali kwa kiwango flani Ukweli wa madia haya ya washikadau wa bongo flavaz. “Kusema kweli natongozwa na mijimama ila nina ‘girlfriend’ na kuhusu bangi, kimtindo si unaelewa? Hata hivyo, nakubali ushauri wa wadau ‘so’ nitakuwa makini.”


kwa upade wake msanii DOGO JANJA ambaye ana  umri wa miaka 15, aliwahi kukumbwa na scandal ya mapenzi alipokubali kutoroshwa usiku na mwanamke mmoja huku akidaiwa pia kuwa mtumizi wa bangi.
Hata hivyo akizungumzia madai haya Dogo Janja anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Makongo aliahidi kuwa makini zaidi.


kinda jipya kabisa katika mziki wa Bongo flavaz DOGO ASLAY ambaye pia ana umri wa miaka 15 na mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Tandika, Dar, anadaiwa kukumbana na usumbufu wa mijimama ya Dar.
Washikadau wa Bongo flavaz kwa sasa wanamtaka Said Fella ‘Mkubwa’ anayemlea kisanii Dogo Aslay kuwa makini.
Fella akubaliana na wadau kwamba kuna tabia amabazo dogo huyu anafaa kukatazwa.
“Naomba tusaidiane na jamii, siyo vizuri kumhusisha mtoto na mambo ya kikubwa kwani umri wake hauruhusu,” alisema Fella.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.


MSANII AMINI HUENDA AKAFUKUZWA THT!

Anakwenda kwa jina la Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, taarifa ni kwamba msela huyu huenda akatimuliwa ndani ya kundi la ‘THT’, kutokana na utovu wa nidhamu.

Akiongea na mapema wiki hii Amini alisema kikubwa kinachotaka kumfukuzisha hapo ni kuchukia tabia za baadhi ya wasanii wa kundi hilo ambao wanajipendekeza kwa mabosi.

Hata hivi Amini alisema si kweli kuwa ana nidhamu mbovu kama inavyodaiwa lakini kutokana hulka yake ya kupenda kusimamia ukweli kwenye kila jambo basi amekuwa akionekana mkorofi.

Mpaka anaongelea swala hili uongozi wa THT ulikuwa unataka kukaa kikao kumjadili kwamba afukuzwe au abaki.

“Yani nimesikia kwamba najadiliwa na uongozi wa kundi ili niweze kufukuzwa lakini kwa upande wangu sioni kama ni tatizo kwa sababu kama kipaji ninacho hivyo nasema kama mimi ni mtovu wa ni nidhamu sawa niko tayari kuondoka,” alisema.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

WASANII WA BONGO FLEVA WANAOTUMIA MADAWA YA KULEVYA WATAJWA.


WASANII WA MADAWA YA KULEVYA WATAJWA.

Kifo cha malkia wa muziki wa Pop, RnB na Soul wa Marekani, Whitney Elizabeth Houston kilichochangiwa na matumizi ya madawa ya kulevya, chaibua mchakato mpya ambapo imepelekea kutolewa kwa orodha ya wasanii wa bongo flavaz wanaodaiwa kwa watumizi wa Mihadarati. Mihadarati iliyotajwa ikiwa ‘unga’, bangi, miraa na aina nyengine.

Habari za chini kwa chini zinadai kuwa kwa sasa mastaa kibao wanatumia madawa ya kulevya huku majina makubwa kama Msafiri Sayai ‘Diouf’, Albert Mangwair, Langa Kileo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Aisha Mbegu ‘Madinda’, Khaleed Mohamed ‘TID’, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’, Abas Kinzasa ‘20%’, David Nyika ‘Daz Baba’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Happiness Thadei ‘Sister P’ na Rose Ndauka yakitajwa.

Katika orodha hii Fid Q ndiye msanii wa pekee aliyejitokeza wazi wazi kukana madai haya.

Huku sanaa ya bongo flavaz ikiimarisha juhudi za kukabiliana na tabia ya utumizi wa Mihadarati miongoni mwa wasanii wa Bongo, wakereketwa wa mziki wa Mombasani pia wahimizwa kuiga juhudi hizi ili kumaliza tabia hii miongoni mwa wasanii wa mkoa wa pwani.

Niwazi kwamba kuna baadhi ya wasanii wa pwani ambao wameonekana wazi wazi wakitumia madawa mbali mbali katika sehemu za burudani hususan kabla ya kufanya performance.

MR.BADO ADONDOSHA PINI JIPYA - "MACHOZI"



MR.BADO ADONDOSHEA MASHABIKI WAKE NYIMBO MPYA - "MACHOZI." AKIMSHIRIKISHA DADAKE

Mr. Bado a.k.a Mzungugiryama

Ni Msanii aliyezaliwa huko  Malindi sehemu ya Watamu katika kaunti ya Kilifi. Alizaliwa mnamo tarehe 15 Desemba mwaka wa 1980. Ni mwana wa msanii Maarufu wa ngoma za kitamaduni za jamii ya Wamijikenda; Mzee Nyerere Wa Konde na Mama Mariam Mohammmed. Ni mtoto wa tano katika familia hii iliyojaliwa watato 10.

Mr. Bado a.k.a Mzungugiryama ambaye majina yake halisi ni Mohammed Said Ngana, alipata masomo yake ya msingi katika shule ya msingi ya Gede Primary School kabla ya kujiunga na shule ya upili ya Barani Secondary School mjini Malindi.

Mr. Bado afichua kuwa usanii wake ulianza kitambo na babake Mzee Nyerere Wa Konde alichangia pakubwa katika yeye kupenda maswala ya mziki na utumbuizaji. Mr. Bado anakumbuka kwa madaha kisa ambacho kilichootesha ari yake ya kuwa mwanamziki. Mr. Bado anasema aliwahi kutumbuiza umati mkubwa akiwa na umri mdogo, ambapo ilikuwa ni mwaka wa 1990 wakati wa matanga ya marehemu nyanyake. Babake ambaye alikua anatumbuiza umati kwa nyimbo zake za kimijikenda alimshika mkono na kumvuta mbele ya umati akimtaka amsaidie katika kutumbuiza watu.

Hata hivyo alianza maswala ya mziki hususan wa kizazi kipya “seriously” mwaka wa 1996 na toka mwaka huo hadi sasa anasema ari yake ya kutaka kufanikiwa kimziki haijawahi kufifia. 

Wimbo wake wakwanza uliomtambulisha kwa mashabiki wa “ngomapwani” anasema ni “Stand By Me “ aliourekodi mwaka wa 2005 katika studio za FP Records chini ya uangalizi wa “Producer”  Fleva, huku akifichua kua show yake ya kwanza ya kutumbuiza mashabiki iliandaliwa katika mkahawa wa Happy Nights mjini Watamu.

Kwa sasa amekuja na kibao kipya kiitwacho “Machozi” akimshirikisha mwanadada kwa jina Shamim a.k.a Shamo, kilichoimbwa kwa lugha ya Kiswahili na kiarabu na kurekodiwa katika studio ya Bado Records, inayopatikana mjini Watamu katika kaunti ya Kilifi mkoani Pwani.

Mr. Bado afichua kuwa mwadada huyu kwa jina Shamim a.k.a Shamo ni dadake mdogo na ushirikiano huu ulikuwa wa kum’introduce kwa “game” ya Mombasani. Mr. Bado afichua kuwa familia yao imejaa wanamziki na mwadada huyu ni nduguye wa pili kujiunga na mziki baada ya kakake mkubwa Nyerere Juniour, ambaye ni msanii wa nyimbo za kitamaduni na babake Nyerer e Wa Konde.

Mr. Bado afichua kuwa karibuni anatarajia kusafiri ng’ambo na angependa kumwacha dadake mdogo akiendeleza ndoto ya mziki, ambayo amefichua kuwa ni sawa na urithi wa kifamilia.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.


MR. BADO & SHAMO - MACHOZI


Contacts:
http://www.facebook/Bado Mzungugiryama
badotalents@gmail.com


LAI AACHILIA WIMBO MPYA – “USIKONDE”




MSANII  LAI  AACHILIA  NYIMBO MPYA KWA JINA  – “USIKONDE”

Msanii wa mziki wa Mombasani Ngala Lai Mwangala maarufu Lai ameachlia ngoma yake mpya kwa jina “Uskonde”.

Lai ambaye pia ni “Producer” wa studio za Crack SoundsMariakani, alizaliwa sehemu ya Mtaani mjini Kilifi katika kaunti ya Kilifi.

Ni mzaliwa wa tatu katika familia ya watoto wanne na ndugu wa tumbo moja na “producer” mwegine mkali Mombasani  producerJay Crack Mfalme wa Crack Sounds - Kilifi.

Alisoma katika shule ya msingi ya Kilifi Primary School kabla ya kujiunga na shule ya upili ya St. Anthony –  Karatina.

Akizungumza na “kaya FlavazLai afichua kuwa alianza mziki “seriously” mwaka wa 2007 kabla ya kupata nafasi ya kurekodi wimbo wake wa kwanza mwaka mmoja baadaye – 2008.Lai asema alirekodi waimbo wake wa kwanza katika studio za FP Records mwaka wa 2008, nyakati hizo studio hiyo inapatikana Watamu.

Wimbo wake wa kwanza ulikuwa unaitwa “Madem” na alikua ameshirikisha wasanii wakali wa nyakati hizo “Majizee

Katika mipango yake ya baadaye Lai afichuaa kuwa anajipanga kumaliza kusomea taaluma ya “Visual and Sound Engineering” katika chuo cha “Home Boys” jijini Nairobi.

Akifunguka kuhusu maisha yake ya kibinafsi Lai asema anam’date mrembo mmoja ambaye wakereketwa wa sanaa ya Mombasani wanamjua kama Mummy D, ambaye pia ni msanii.

Asipokuwa mitambano, Lai asema yeye hupenda kuhudhuria masomo ya bibilia na kufichua kuwa kila jumapili hushiriki maombi katika kanisa la Royal Tarbanacle na pastor wake ni Shadrack Ndune.

Akizungumzia “game” ya Mombasani, Lai ataja ukosefu wa “seriousness” miongoni mwa  wasanii wa mombasani kama sababu kuu ya sanaa kutopiga hatua za kimaendeleo licha ya uwepo wa wasanii wenye vipaji.

“Watu wengine waingia “game”na hawajajipanga ama hawako “serious”. Mtu ataingiaje “game” na 4000/= pesa  za kurekodi! Nairobi msanii chipkizi anaingia game na “manager” na “budget” kubwa ya hela kufadhili mwanzo wa “career” yake. Ni kama anafanya "investment" ya biashara. Huku kwetu watu wanafanya mziki kama “fun”…….ndio maana mziki ama sanaa ya Mombasa nayo inawachukulia”fun” pia”, akamalizia.

Akizungumza kuhusu wimbo ake mpya Lai asema wimbo huu unalenga kila mmoja katika jamii na unawapa moyo wanajamii licha ya hali ngumu za kimaisha.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.


LAI - USIKONDE


Contacts:
http://www.facebook/Lai Mwangala
laimwangala@yahoo.com

Saturday, February 18, 2012

"DUDUBAYA APANGA KUHAMA DAR"



DUDUBAYA KUHAMA DAR ES SALAAM KARIBUNI.

MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini aka Dudubaya anaeishi area 88.4 Dar es salaam nchini Tanzania,  ametangaza rasmi kupitia mtandao mmoja wa kijamii kwamba anajipanga kuihama Dar es Salaam na kwenda kuishi kwao Kiseza huko Mwanza  katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Dudubaya asema sababu mbili kubwa zinazomfanya kuuhama mji mkuu wa Tanzania Dar es Salaam na kuelekea mkoa wa Mwanza ni  joto na jam za barabarani, ambazo amedai humchelewesha kila mara .

Dudubaya ambae alianza maisha ya kujitegemea jijini Dar es salaam miaka saba iliyopita, amesema kwa sasa anakaribia kumalizia nyumba yake anayoijenga  nyumbani kwao Mwanza, ambayo anadai imemgharimu shilingi milioni kumi pesa za Tanzania.

Kwa sasa Dudubaya anamiliki  kampuni moja inayojihusisha na kuuza madirisha na milango ya mbao, pamoja na kampuni ya kuandaa show za wasanii kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania hukuakijihusisha na ulimwengu wa filamu za kibongo pia.


Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

Friday, February 17, 2012



“RUDI NYUMBANI MWANANGU”

Mama wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ray C ambaye majina yake kamili ni Rehema Chalamila amtaka mwanaye kurudi kwao nchini Tanzania.

 Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Ray C mamake Ray C hajafurahia kitendo cha mwanaye kuhamia jijini Nairobi na akamtaka kurudi  Bongo ili awe karibu naye.

Kulingana na nduguye Mamayake anataka Ray C arudi kuja kufanya shughuli zake za kimuziki Bongo kwani hufurahi kumuona mara kwa mara .

Mwanzoni mwa wiki hii mamake Ray C huyo alisikika akizungumza katika Kipindi cha stesheni mmoja nchini  Tanzania na alikiri kutamani kwake kumuona mwanawe amerudi nyumbani.

Mamake Ray C asema hakumpa Ray C baraka za kuja kuishi Kenya na akasistiza angependa mwanae arudi nchini Tanzania na kumuimbia mungu.

Kwa sasa Ray C anaishi nchini Kenya na kufanya shughuli zake za kimuziki nchini jijini Nairobi na hivi karibuni alizindua bendi  yake.

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.

PROFESA JAY A'LAUNCH FAN PAGE”

PROFESA JAY  A'LAUNCH "FAN PAGE” YA SIMU YA MKONONI



“Jina langu limevuma, Kwenye mitaa.
 Jina langu lina hadhi ya ki-superstar.
 Jina langu…..”

Hii ni mistari kutoka kwenye wimbo wa msanii Profesa Jay kwa jina "Jina Langu"
Ni miongoni mwa wa wasanii mahiri na waanzilishi wa Bongo Flava na anayesifika hata hapa kwetu pwani.

Profesa Jay au Prof Jiizeh kama wengine wanavyomwita

Alizaliwa jijini Dar-es-salaam tarehe 29 December 1975. Ni mtoto wa sita kati ya watoto tisa wa Mzee Leonard Steven Haule na Mama Rose Majanjara. Baadaye akasoma Ukonga Primary School kabla hajaelekea mji kasoro bahari(Morogoro) kusoma Kigurunyembe Secondary na baadaye Mbeya Lutengano High School.

katika maisha yake ya miaka 15 ya kimziki amewahi kushinda tuzo za mziki nyingi.
Albums:
Machozi Jasho na Damu 2001
Mapinduzi Halisi 2003
J.O.S.E.P.H 2006
Aluta Continua 2007

Tuzo:

Alizoshinda:

 2004 Tanzania Music Awards (Kilimanjaro Music Awards)- Best Hip Hop Album ("Mapinduzi Halisi")
2006 Tanzania Music Awards - Best Song (Nikusaidiaje)
2006 Kisima Music Awards - Best Tanzanian Song (Nikusaidiaje)
2007 Kisima Music Awards - Best Ugandan Song (Sivyo Ndiviyo with Chameleone)
2007 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Best Male Artist (Tanzania)
2009 Tanzania Music Awards - Best Songwriter

Uteuzi:

Nominated 2008 MTV Africa Music Awards - Best Hip Hop.
Hivi karibuni ameweza ku’launch “fan page” yake ambayo inalenga kumuunganisha na mashabiki wake moja kwa moja kupitia simu ya mkononi.

To Follow Professor Jay on SMS, Text PROFJ leave the space, Write your name Then send it
to 15678. Updates are FREE.

“Ni fan page kwa kutumia sms maana kuna wengine hawana uwezo wa kutumia twitter, BBM au Facebook so hii unaweza ukachat nami moja kwa moja kama tunavyofanya kwenye mitandao mingine!! Ninajua umuhimu wa mashabiki wangu na ninawahitaji sana wote NO MATTER WHAT!! so mwenye swali, maoni , Pongezi au DEAL yeyote inayohusu muziki TUWASILIANE hapa”

Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.