PROFESA JAY A'LAUNCH "FAN PAGE” YA SIMU YA MKONONI
“Jina langu limevuma, Kwenye mitaa.
Jina langu lina hadhi ya ki-superstar.
Jina langu…..”
Hii ni mistari kutoka kwenye wimbo wa msanii Profesa Jay kwa jina "Jina
Langu"
Ni miongoni mwa wa wasanii mahiri na waanzilishi wa Bongo Flava na
anayesifika hata hapa kwetu pwani.
Profesa Jay au Prof Jiizeh kama wengine wanavyomwita
Alizaliwa jijini Dar-es-salaam tarehe 29 December 1975. Ni mtoto wa sita kati
ya watoto tisa wa Mzee Leonard Steven Haule na Mama Rose Majanjara. Baadaye
akasoma Ukonga Primary School kabla hajaelekea mji kasoro bahari(Morogoro)
kusoma Kigurunyembe Secondary na baadaye Mbeya Lutengano High School.
katika maisha yake ya miaka 15 ya kimziki amewahi kushinda tuzo za mziki nyingi.
Albums:
Machozi Jasho na Damu 2001
Mapinduzi Halisi 2003
J.O.S.E.P.H 2006
Aluta Continua 2007
Tuzo:
Alizoshinda:
2004 Tanzania Music Awards (Kilimanjaro Music Awards)- Best Hip Hop Album
("Mapinduzi Halisi")
2006 Tanzania Music Awards - Best Song (Nikusaidiaje)
2006 Kisima Music Awards - Best Tanzanian Song (Nikusaidiaje)
2007 Kisima Music Awards - Best Ugandan Song (Sivyo Ndiviyo with Chameleone)
2007 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Best Male Artist (Tanzania)
2009 Tanzania Music Awards - Best Songwriter
Uteuzi:
Nominated 2008 MTV Africa Music Awards - Best Hip Hop.
Hivi karibuni ameweza ku’launch “fan page” yake ambayo inalenga
kumuunganisha na mashabiki wake moja kwa moja kupitia simu ya mkononi.
To Follow Professor Jay on SMS, Text PROFJ leave the space, Write your name
Then send it
to 15678. Updates are FREE.
“Ni fan page kwa kutumia sms maana kuna wengine hawana uwezo wa kutumia
twitter, BBM au Facebook so hii unaweza ukachat nami moja kwa moja kama
tunavyofanya kwenye mitandao mingine!! Ninajua umuhimu wa mashabiki wangu na
ninawahitaji sana wote NO MATTER WHAT!! so mwenye swali, maoni , Pongezi au
DEAL yeyote inayohusu muziki TUWASILIANE hapa”
Kwa mengi Zaidi usikose kumskiza Sista Shaniz a.k.a Anti-Virus katika "Show Nambari Moja Mkoani Pwani™" - "Kaya Flavaz®" ndani ya RADIOKAYA 93.1Fm Msa 99.7Mlnd - "Kitovu Cha Umoja Wa Pwani ™.